Naibu
Waziri wa Maji,Mh Amos Makala akiongea na vyombo vya habaria katika
ziara yake ya kikazi jijini hapa kwa lengo la kutembelea miradi ya maji
iliyokuwa na changamoto kubwa ya upotevu wa maji inayosababishwa na
uchakavu wa miundombinu na wizi wa maji
Naibu
Waziri wa Maji,Mh Amos Makala kulia akiwa anasikiliza maelezo kutoka
kwa Eng wa maji Bw.Mohamed Ismail katika eneo la chanzo cha maji mto
nduruma katikati niKaimu mkurugenzi wa mamlaka ya maji Arusha Eng.Fabian
Maganga
Muonekano wa maporomoko ya maji mto nduruma ni chanzo kikubwa kinachotegemewa Mkoani Arusha katika huduma ya maji
Askari anayelinda eneo hilo
Naibu
Waziri wa Maji,Mh Amos Makala wa nne kulia akiwa anateta jambo katika
moja ya maporomoko ya maji ijulikanayo kama mto nduruma wengine ni
watumishi wa mamlaka hiyo
Kulia
aliyesimama ni Makamu mwenyekiti wa bodi ya maji Mkoa wa Arusha
Bw.Joshua Kileo akiwa anazungumza wakati Naibu Waziri wa Maji,Mh Amos
Makala alipokuwa anazungumza na watumishi wa mamlaka ya maji Arusha
Naibu
Waziri wa Maji,Mh Amos Makala akiwa anaangalia moja ya ujenzi wa chanzo
kipya cha maji katika eneo la kisongo ambacho kitasaidia wananchi wa
eneo hilo kupata huduma ya maji
Hii ni mitambo ya kuwekea maji dawa
Naibu Waziri wa Maji,Mh Amos Makala akiangalia moja ya kisima cha maji katika kijiji cha Olturuto wilaya Arumeru
Naibu Waziri wa Maji,Mh Amos Makala akionge akatika moja ya chanzo cha maji kinachotengenezwa eno la kisongo Mkoa Arusha
Naibu Waziri wa Maji,Mh Amos
Makala amewataka wananchi wa Mkoa wa Arusha kuendelea kuwafichua wale
wote wanaoshiriki katika wizi wa maji ili waweze kuchukuliwa hatua kali
za kisheria
Alitoa wito huo jana wakati akiwa katika ziara yake ya kikazi
jijini hapa kwa lengo la kutembelea miradi ya maji iliyokuwa na
changamoto kubwa ya upotevu wa maji inayosababishwa na uchakavu wa
miundombinu na wizi wa maji
Waziri Makala alisema kuwa
serikali inafanya jitihada ya kuboresha huduma ya maji ikiwa nipamoja na
kuboresha miundombinu,kukomesha wizi wa maji kwa kutoa elimu kwa
wananchi
“Wizi wa kujiunganishia maji
katika maeneo mbalimbali hapa nchini upo lakini kwa sasa tunaoparesheni
ya kuwasaka wale wote wanaotumia maji bila kulipa watambue kuwa kwa
kufanya hivyo ni kinyume na sheria”alisema Makala
Aidha katika moja ya chanzo
kikubwa cha maji mto nduruma alisema kuwa chanzo hicho kinategemewa kwa
mkoa wa Arusha hivyo alitoa pongezi kwa mamlaka ya maji kwa kuwa
wabunifu
Naye Kaimu mkurugenzi wa mamlaka
ya maji Arusha Eng.Fabian Maganga alisema kuwa kwa hivi karibuni
walikuwa na zoezi la ukaguzi wa nyumba hadi nyumba na kufanikiwa
kuwakamata watu wanaohujumu mamlaka hiyo takribani 750 hivyo zoezi hilo
bado ni