Marafiki
wa aliyekuwa mshiriki wa Miss Tanzania 2013 akitokea Miss Ilala, Martha
Gewe wakiwa na huzuni.KWELI kifo hakina huruma jamani! Mshiriki wa Miss
Tanzania 2013 akitokea Miss Ilala, Martha Gewe, mkazi wa Tabata
Segerea, Dar amefariki dunia baada ya kuugua ghafla, Ijumaa Wikienda
linakupa zaidi.
Martha
amekutwa na mauti katika Hospitali ya Mkoa wa Ilala, Amana jijini Dar
es Salaam, Ijumaa iliyopita ambako alikimbizwa baada ya kuugua na
madaktari walibaini kwamba, malaria ilipanda kichwani. Marehemu Martha
Gewe enzi za uhai wake. Watimanywa usiku wa kuamkia leo, kule jijini
London, Uingereza alifurukuta kugombea Taji la Miss World! Habari zaidi
zinasema kuwa mrembo huyo hakuwa akisumbuliwa na ugonjwa wowote huko
nyuma na alionekana mwenye afya njema huku mipango yake ikiwa imelenga
jinsi atakavyoisherehekea Sikukuu ya Krismasi. “Lakini Jumatano
iliyopita alianza kuumwa, alisema anahisi homa ambayo baadaye ikabainika
ni malaria.