Hakimu David Mwita wa Mahakama ya
mwanzo ya maji ya chai ameahirisha hadi december 24, shauri la
kesi inayomkabili Mbunge wa Jimbo la Arumeru mashariki Joshua Nassari
(CHADEMA), kwa tuhuma za kuharibu mali ya uma kwa kuichoma yenye
dhamani ya shilingi laki mbili (bendera ya CCM),pamoja na kumteka mtu
na kumtishia kwa bunduki tukio ambalo anatuhumiwa kufanya december
15 mwaka huu
mahakama hiyo imeweza kumuachia mbunge
huyo mara baada ya kutimiza mashariti ambapo shariti la kwanza ni
kuwa na wathamini wa tatu ambao wanamali zisizo amishika zenye
dhamani ya shilingi milioni moja na nusu kila mmoja.
Katika kesi hiyo inayomkabili mbunge
huyo ambayo mlalamikaji wa kesi hiyo akiwa ni mtu binafsi hakimu wa
kesi hiyo mara baada ya kusikiliza mashitaka hayo alichukuwa nafasi
ya kuhairisha kesi hiyo adi december 24 ambapo kesi hiyo itatajwa
tena kwa mara nyingine.
Akiongea mara baada ya kuairisha kesi
hiyo wakili wa mbunge huyo wa Arumeru mashariki James Ole milya
alisema kuwa amesikitishwa sana na tukio la mahakama hiyo kumpa
mashariti makubwa mteja wake kwani kesi yake ilikuwa haitaji
mashariti makubwa hivyo .
Aidha alisema kuwa mbali na kupewa
mashariti hayo angependa kesi hiyo ipelekwe katika mahakama ya
wilaya ili yeye kama wakili wa mbunge huyo aweze kumtetea kwani
katika mahakama ya mwanzo hairuhuu kuweka wakili.
“unajua kwakweli mbali na hivyo
pamoja kuwa sio jamuhuri imemshitaki mh Nasari bali ni mtu binafsi
lakini nasikitika sana kwa mashariti ambayo wameweka ,kwani ata bila
ao wathamini watatu wakiwa na kitu kisichoamishikika chenye dhamani
ya shilingi milioni moja na nusu,huyu ni mbunge ambapo angeweza
kujidhamini ata yeye mwenyewe kwani mtu huyu ni kioo cha jamii na
awezi kukimbia sehemu yoyote kwanini wasinge mpa mdhamana mapema
mpaka apate wadhamini hawa na mashariti haya”alisema Milya
Aidha alisema kuwa anashangazwa sana na
maamuzi haya kwani kuna mtu ambaye amemzalilisha mwanamke ambaye
alikuwepo mahakamani hapo na akamvua mwanamke huyo nguo lakini yeye
alishangazwa sana kwa mtuhumiwa wa kosa ilo la uzalilishaji yeye
kupewa mashariti mapesi ya kuwa na mdhamini mmoja na kutoa laki tano
laikini mbunge yeye amepewa mashariti ya kuwa na wadhamini watatu
ambao wanamalizi zenye dhamani ya shilingi milioni moja na nusu uku
akitilia shaka kuwa katika kesi hii wanahisi kuna chama cha siasa
kinachangia kuongeza nguvu.
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia