Spika wa Bunge la Afrika Mashariki(Eala)Daniel Kidega |
Spika mpya akila kiapo bungeni leo |
Spika akiongozwa na askari wa Bunge kuingia bungeni. |
Aliyechaguliwa bila kupingwa ni Daniel Kidega kutoka nchini Uganda kuchukua nafasi ya Mh Magreth Zziwa aliyeondolewa kwenye kiti hicho siku ya jumatano wiki hii baada ya wabunge wenzake kumtuhumu kushindwa kuongoza chombo hicho muhimu.
Awali taarifa za kuaminika zilizoufikia zilisema majina manne kutoka wabunge wa Uganda waliochukua fomu walikua ni Daniel Kidega,Susane Nakahuki,Chris Opoka Okumu na Mike Sebaru.
Hata hivyo baadhi yao hawakurudisha fomu ya kuwania kunyanganyiro hicho huku mh Chris akiondoa jina lake na kumwachia Dan Kidega kupita bila upinzani.