Jumla
ya timu 34 kutoka nchi za Kenya,Uganda na Tanzania zimeanza kumenyana
katika michuano ya Kombe la Chipukizi lililoanza kutimua vumbi jana
katika viwanja vya shule ya kimataifa ya Moshi na TGT vilivyopo nje
kidogo ya jiji la Arusha.
Kwa
mujibu wa taarifa iliyotolewa na mwandaaji wa michuano hiyo ambaye pia
ni mkurugenzi wa kituo cha Future Stars Academy,Alfred Itaeli alisema
kuwa timu hizo ni 7 kutoka Kenya,9 kutoka Uganda na timu 18 kutoka
nchini Tanzania.
Alisema
kuwa timu hizo zimegawanyika katika makundi ya umri chini ya miaka
U-10,U-12,U-14,U-16 na U-18 ambapo mechi za awali zinataraji kuchezwa
katika uwnaja wa kumbukumbu wa Sheikh Amri Abeid uliopo jijini Arusha.
Itaeli,alisisitiza
ya kuwa vigezo vyote vya kubaini umri sahihi kwa washiriki
vimezingatiwa ikiwa ni pamoja na ukuhakiki vyeti mbalimbali vya kuzaliwa
kwa wachezaji huku akisisitiza ya kuwa mtanange wa fainali unataraji
kupiigwa katika uwanja wa shule ya kimataifa ya Moshi(ISM).
Aliwataka
wakazi wa Arusha na viunga vyake pamoja na makocha mbalimbali
wanaofundisha timu za vijana kujitokeza kwa wingi kushuhudia vipaji
mbalimbali katika michuano hiyo ambapo alitaja lengo kuu la mashindano
hayo ni kuibua vipaji vya soka kwa watoto wadogo hapa nchini.
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia