BREAKING NEWS

Tuesday, December 9, 2014

DK SLAA AWALILIA WAKULIMA KARATU, NGORONGORO

MBUNGE Karatu, Dk Wilbrod Slaa, ameitaka Serikali ya Mkoa wa Arusha kuanzisha vyama vya misingi vya ushirika katika Wilaya za Karatu na Ngorongoro, ili viweze kuwasaidia wakulima wa wilaya hizo.

Dk Slaa, alisema hayo  kwenye kikao cha Kamati ya Ushauri ya Mkoa wa Arusha kilichofanyika kwenye Kituo cha Kimataifa cha Mikutao (AICC) kujadili utekelezaji wa mikakati ya maendeleo ya Mkoa wa Arusha.

Alisema wakulima wa wilaya hizo kwa sasa wamekuwa na wakati mgumu wa kupata pembejeo za kilimo mbegu bora pamoja na masoko ya mazao yao kutokana kukosekana kwa vyama imara vya ushirika kwenye wilaya hizo.

Alisema kwa kuwa wakulima hao wanatumia Chama cha Ushirika cha Mkoa wa Manyara (RIVACU), hawanufaiki na chama hicho kwani makao makuu ya chama hicho yapo mkoani Manyara na kwamba wakulima wa Karatu Ngorongoro hawashirikishwi kwenye vikao na mikutano muhimu ya chama.

“Kwa muda mrefu wakulima wetu wamekuwa wanakosa haki yao ya kimsingi japokuwa wamekuwa mstari wa mbele katika uzalishaji wa mazao ya mahindi na vitunguu kwa wingi na kuwa tegemeo katika Mkoa wa Arusha na hata mikoa mingine nchini, hivyo imefika wakati wa serikali kushughulikia jambo hili haraka,” alisema Dk Slaa.

Hoja hiyo pia iliungwa mkono na Mkuu wa Wilaya ya Ngorongoro, Jovika Kasunga ambeye pia alisema kuwa wilaya hizo hazina benki za kutosha na kutoa mfano wilaya yake ina benki mojo ya NMB.

Share this:

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

 
Back To Top
Copyright © 2014 MOUNT KILI NEWS. Designed by OddThemes | Distributed By Gooyaabi Templates