wapiga kura sehemu mbalimbali
Chama
cha mapinduzi kimeweza kuibuka kadedea katika uchaguzi wa uwenyekiti wa
mitaa katika mitaa yote iliopo ndani ya mkoa wa Arusha baada ya
kuvishinda vyama vingine vya upinzani .Akitangaza
matokeo ya uwenyeviti wa mitaa mkurugenzi wa jiji la Arusha Iddi Juma
alisema kuwa mpaka sasa uchaguzi wa uwenyekiti umekamilika katika mitaa
yote na vituo vyote isipokuwa kituo kimoja ambacho uchaguzi wake
utarudiwa siku ya kesho.Alisema
kuwa katika uchaguzi huu jumla ya wananchi 1,13909 walijiandikisha
kupiga kura na jumla ya vyama sita vilisimamisha wagombea katika kila
mtaa ambapo alitaja vyama ambavyo vilisimamisha wagombea kuwa ni pamoja
na ACT,chama cha mapinduzi CCM,NCCR mageuzi ,CUF pamoja na TLP .Akitaja
matokeo ya uwenyekiti wa mitaa alisema kuwa ccm imeweza kuongoza kwa
kupata mitaa mingi zaidi ambapo alisema kuwa CCM imeweza kupata kura 78
ambapo kati ya kura hizo kura sita ni za kupita bila kupigwa, ikifuatiwa
na chadema ambao wana kura 75 ,ACT ikiwa aijapata kura ,NCCR ikiwa
aijapata kura ,CUF ikiwa aijapata kura pamoja na TLPAidha
alibainisha kuwa jumla ya vituo 154 vilikuwa wepo kwa ajili ya kupigia
kura na vyote vimekamilisha uchaguzi isipokuwa kimoja ambapo kilifutiwa
matokeo hayo na kulazimika kurudiwa ambapo alisema kuwa katika kituo
hicho uchaguzi utarudiwa hapo kesho .mpaka
sasa uchaguzi wa uwenyekiti umemalizika ila tumelazimika kurudia
uchaguzi katika vituo vitatu ambapo katika vituo hicho kituo kimoja
ambacho ni cha Oysterbay uchaguzi utarudiwa kwa watu wote na maanisha
uchaguzi wa kuanzia kwa mwenyekiti wa mtaa ,wajumbe watano pamoja na
wajumbe watatu wa viti maalumu huku katika kituo cha AICC -Sekei
uchaguzi utarudiwa kwa wajumbe watatu wa viti maalumu ambapo hii
inatokana na kura za kufungana kwani wote walipata 31 kwa 31 na katika
kituo cha Oldpolisi line ambapo napo uchaguzi utarudiwa kwa watu wawili
ambao nao pia ni wajummbe wa viti waamaalu walifungana kwa kura 64 kwa
64.
Juma
alisema katika uchaguzi wakesho ambao wanarudia wamejipanga vizuri
kusimamia kwani nguvu zote wanazielekeza katika vituo hivyo ambapo
alibainisha kuwa katika kila kituo kutakuwa na wasimamizi nane pamoja na
ulinzi wa kutosha .
Aidha
alitumia fursa hii kuwashukuru wananchi wate na viongozi kwa kufanya
uchaguzi wa amani na kistarabu pamoja na kuvumiliana huku akiongeza
kuwaanamatumaini utulivu huu na uvumilivu walionyesha utaendelea hata
katika vituo hivi ambavyo vinarudiwa.