Ticker

6/recent/ticker-posts

SEREKALI YATAKIWA KUBORESHA MAZINGIRA YA WAKULIMA WA KILIMO CHA MBOGAMBOGA, MATUNDA NA MATUNDA

Na Woinde Shizza,Arusha

 

Serekali imetakiwa kuboresha mazingira  yakuwezesha biashara ili kuweza kuongeza uwekezaji wa sekta binafsi kwenye sekta ya kilimo .

 

kufanya hivyo kutasaidia kupunguza  tatizo la ajira ambalo ndio kero kubwa inayosumbua vijana wengi hapa nchini kwani   sekta hii ya  kilimo kupitia kilimo cha mboga mboga matunda na mauwa (horticuture) kinawezesha vijana wengi kujiajiri na kutoa ajira kwa  vijana wengine.

 

Haya yalibainishwa jana  na naibu afisa mtendaji mkuu (maendeleo) wa asasi kilele ya kilimo horticuture (TAHA) Anthony  Chamanga  wakati akiongea  na waandishi wa habari ofisini kwake ambapo alisema kuwa iwapo kilimo hichi kitatiliwa mkazo basi kitamnufaisha mwananchi pamoja na nchi kwa ujumla kwa kumpatia kipato.

 

Alisema kuwa  iwapo serekali itasaidia  kuboresha mazingira  ya kuwazesha  biashara itasiadia kwa kiasi kikubwa kupunguza tatizo la ajira  pamoja na kuongeza patao la taifa kwani wakulima watalima na mazao yatakayo patikana yatauzwa na kuwasaidia kuingiza kipato cha mkulima pamoja na kuongezea pato la taif a kwani mkulima atalipa kodi na kuileta nchi   faida kwa ujumla.

 

Aidha pia aliiomba serekali  kusaidia sekta  hii kwa kuboreshas miundo  mbinu ya umwagiliaji pamoja na  upatikanaji wa masoko katika sekta ya horticuture.

 

Alibainisha kuwa ukimwezesha mkulima wa horticuture  kulima  kilimo cha kisasa na kitaalamu hii itamuezesha mkulima kuweza kuifadhi mazao yake baada ya kuvuna ili aweze kupata bei nzuri sokoni na pia itamuezesha mkulima kuweza kupata mnunuzi mapema na moja kwa moja  bila ya kupitia  kwa madalali.

 

Alisema kuwa   mbali na changamoto hiyo pia kunachangamoto kubwa ya mabadiliko ya hali ya hewa  kwani kilimo hicho kinaitaji maji mengi na kilimo hicho akiwezi kufanyika sehemu ambayo aina maji hivyo ni muhimu wakulima kufaata sheria kanuni na kununua mbegu bora ambazo zinaeza kutunza mazingira  na ambazo zitahakikisha  matumizi sahii ya maji.

 

“navyosema kutunza mazingira na matumizi sahii ya maji ni kwamba wakulima wanapaswa watumie mbinu bora  zitazotunza  mazingira na ambazo zinatunza  matumizi ya maji  na h ivyo tunapaswa tutumie teknolojia ya kutumia  maji kwa kuifadhi mfano tunaweza kutumia umwagiliaji wa matone ili kuweza kutunza maji na kutumia maji kidogo  au pia tunaweza kuifadhi maji kwa kutengeneza bwawa ambalo linaplastiki ndani  na sisi wakulima pia tunajua kunasheria ya matumizi ya maji hivyo ni muhimu kila mkulima kufuata sheria ya maji na kupata kibali kabla ya kuanza kutumia au kuifadhi maji hayo”alisema Chamanga

 

Chamanga aliitaka serekali  ipitie tena sera ya kilimo kwani baadhi ya vifungu vilivyopo katika sera hiyo avijakaa vyema  na vingine avijajitosheleza kikanuni   na vinapelekea  kuwaumiza wakulima wa horticulture.

 

Alisema kuwa upatikanaji wa pembejeo  umekuwa mgumu sana haswa kwa upande wa pembejeo za kisasa pamoja naupatikanaji wa madawa  ya mimea imekuwa mgumu kutokana  na baadhi ya sera hizo hivyo aliisihi serekali  kupita tena sera hizi na kuzirekebisha ili kumuezesha mkulima  kufanya kilimo cha kisasa na chenye tija kitakachomnufaisha mkulima pamoja na serekali kwa kuongeza kipato.

Post a Comment

0 Comments