Flag this messageSHERIA YA UCHAGUZI 1985 IREKEBISHWE-ANGONET



Wadau wa haki za binadamu wakiongea na waandishi wa habari wa kwanza kushoto ni Elinami Mungure


Mtandao unaounganisha mashirika yasiyo ya kiserikali mkoani arusha(ANGONET)umeitaka serikali kuiangalia upya sheri ya uchaguzi ya mwaka 1985 na kupunguza mapungufu yake ili kuweza kumaliza migogoro inayojitokeza ndani ya vyama vya siasa.

Mtandao huo umebaini kuwa kuna mapungufu mengi katika sheria hiyo pamoja na kubadilika mara kwa mara pamoja na sheria za chaguzi za serikali za mitaa na kanuni zake.

Changamoto hiyo imetolewa mwishoni mwa wiki na mratibu wa ANGONET mkoani hapa Petro Ahham.alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kwa kutokana na vurugu za kisiasa zilizojitokeza januari tano mwaka huu na kusababisha kuumia kwa raia na hata wengine watatu kufariki dunia.

Mratibu huyo alisema kuwa katika Ibara ya 20 ya katiba ya jamuhuri ya muungano wa Tanzania haki ya watanzania kujumuika na kukutana imetolewa kama haki ya msing ila haki hiyo inanyang’anywa kwa sheria ya jeshi la polisi na vikosi vya usalama katika sura ya 322 ya mwaka 2002 kifungu cha 43(1).

“kutokana na machafuko yaliyotokea hapa mkoani kwetu kwakweli tukiwa kama wanamtandao wa mashirika ya kiserikali tunalaani vikali kwa kitendo hiki na hutaruhusu hali kama hii ijitokeze tena kwani ni kushusha hadhi ya mkoa wetu ambao unasifika kwa kuwa na vivutio vingi vya kitalii na kuitwa “Geneva of Afrika”alisema mratibu huyo.

Aidha alisema kuwa mara baada ya kufanya tafiti zao waligundua kiini cha kutokea kwa vurugu hizo kuwa ni uchaguzi wa meya wa mkoa huo ambapo utata wa katika uhalali wa wabunge wa viti maalumu kutoka chama tawala(CCM)Mary Chatanda na Rebecca Mngondo viti maalumu wa CHADEMA katika mchakato mzima wa kumchagua meya wa arusha kulitokea mkanganyiko wa sheria.

Alisema kufuatia mkanganyiko huo ulitoa mwanya wa kuruhusu majibizano baina ya vyama hivyo viwili vya CCM na CHADEMA,hadi kusababisha kufanywa kwa maandamano.

“katika ibara ya 59(1)na 69(1)sheria ya uchaguzi 44, 81, 86 kifungu kidogo cha 6 na kifungu cha 24 1(d ) ya sheria ya serikali za mitaa mamlaka za miji na 3 ya mwaka 2006,kanuni ya 23 na 30(4) ya kanuni za bunge ya mwaka 2007 ndizo zilizotumiwa kutoa uhalali wa wabunge hawa kwa mujibu wa naibu katibu wa bung end.Eliakim P. Mrema kwa barua yake kumb. CEB/77/155/01/79 ya Disemba mwaka 2010.”alisema Ahham.

Alitoa wito kwa serikali ili kunusuru hali hiyo ya vurugu za kisiasa kutotokea tena basi ni vyema tafsiri ya majumuiko ya sheria hizo ziangaliwe kwa makini zaidi kwani zinadhihirisha udhaifu mkubwa wa sheria na kuzua maswali mengi kuliko majibu yake.

Aliendelea kwa kusema kuwa mtandao huo pia umebaini pia sheria za serikali za mitaa hazitoi muongozo kuhusu kumchagua Meya ila waziri wa TAMISEMI ndiye aliyepewa mamlaka ya kutunga kanuni za kudumu za uchaguzi huo.

Alisema pia kumekuwepo kwa udhifu mkubwa wa kiutendaji na watendaji ndani ya serikali na taasisi zake ikiwemo tume ya uchaguzi,TAMISEMI,Msajili wa vyma vya siasa na vyombo vya ulinzi na usalama(polisi na usalama wa Taifa).

Mratibu huyo alisema bado kuna muingiliano kati ya Bunge,TAMISEMI na Tume ya uchaguzi katika utambuzi wa uhalali wa wabunge viti maalumu na utatuzi wa migogoro kamahiyo.

“Hali hiyo ilifikiwa wakati TAMISEMI na Tume ya uchaguzi wanatupiana mzigo wa kutatua uchaguzi hasa ikizingatiwa waziri Mkuchika ni kiongozi wa chama cha mapinduzi(CCM) huku muingiliano wa mamlaka ulionekana wazi katika kutoa maamuzi kati ya OCD,RPC na IGP kuhusu kuruhus au kutoruhusu maandamano ya CHADEMA”alisema.

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

Previous Post Next Post