AFC WAPEWA DOZI NYUMBANI



timu ya AFC ikichuana na African lyon jana katika uwanja wa sheikh Amri Abeid jijini hapa

Matumaini ya timu ya AFC kubaki ligi kuu yamezidi kuingia dosari mara baada ya kupigwa kipigo cha bao 1-0 katika uwanja wa njumbani wa Shekh Amri Abeid na wageni wao African Lyon.

Bao ambalo limealetea huzuni kubwa na kuwavunja moyo washabiki wa mpira wa miguu wa mkoa wa Arusha waliouthuria kushuhudia mechi hii ambayo ni ya ufunguzi wa mzunguko wa pili lili ingizwa kimnyani na Hamis Thabit kunako dakika ya nane ya mchezo mara baada ya mchaji huyu kuweza kuwachenga na kuwaacha wamebutwaa walinzi wa timu ya AFC.


Mechi iliendelea na iliendelea na hadi kipindi cha kwanza kumalizika wenyeji AFc walikuw ahawaja bahatika kupata bao hata moja hali ya kwamba waliporudi katika kipindi cha pili walijitaidi kucheza kwa kasi lakini walijikuta wakipoteza mipira mingi mara tu walipo fika katika lango la timu ya African lyon.

Ilipotimu kunako dakika ya 87 ya mchezo mchezaji wa timu ya AFC Jumanne Manyiro aliweza kuyaona mashindano haya machungu mara baada ya kuzawadiwa kadi nyekundu na muhamuzi aliyekuwa akichezesha mechi hii Ibrahimu Kidiwa kutoka Mkoani Kilimanjaro mara baada ya kumchezea vibaya mchezaji wa Afrika lyoni.

Gazeti hili lilizungumza na kocha wa timu ya AFC Rashidi Chama kuhusiana na mechi hii yeye alisema kuwa mechi ni nzuri na hawezi kuwalaumu wachezaji kwani ndo kwanza wameingia kambini juzi(jana)hivyo ilo awezi sema.

Alisema kwakuwa ndo amekabidhiwa timu tu na katika mechi ya leo ameona mapungufu mengi yeye akiwa kama mwalimu na atayarekebisha na anaimani kuwa timu yaweza panda daraja.

pia aliwatupia lawama waamuzi wa mechi hii na kusema kuwa anawaomba viongozi wa TFF wawaangalie sana waamuzi ambao wanawatuma kuchezesha mechi hizi kwani wengi wao hawafuati sheria akitupia lawama zaidi waamuzi wa leo.

Kwa upande wa kocha wa timu ya Afrikan lyon Jumanne Chale yeye aliwatupia lawama waamuzi wa mechi hii akisema kuwa walikuwa hawafuati sheria kama zinavyotakiwa na kusema kuwa walikuwa wanaona makosa lakini hawayafanyiii kazi.

"mechi ilikuwa nzuri vijana wangu wamejitaidi ila hawa waamuzi wa leo kweli hawakuwa makini na maamuzi yao ambayo walikuwa wanayatoa hivyo wabadilike na hawa viongozi wa TFF waangalie sana waamuzi wao"alisema Jumanne.

Alisema kuwa wao wanauhakika wa kubaki ligi kuu kwani mpaka sasa wana jumla ya pointi 13 ambazo wanauhakika wa kuendelea kuziongeza katika mechi zao zote ambazo watacheza.

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

Previous Post Next Post