Naibu waziri wa Aridhi ,nyumba na maendeleo na makazi MH.Godluck Ole Medeye akiwa anacheza ngoma pamoja na wamasai mara baada ya picha ya pamoja
washiriki wa semina ya chama cha wabunifu wa majengo na nyumba Tanzania wakiwa katika picha ya pamoja
Naibu waziri wa Aridhi ,nyumba na maendeleo na makazi MH.Godluck Ole Medeye akifungua mkutano wa semina ya wasanifu wa majengo
washiriki ya semina hiyo wakiwa makini kusikiliza
Imebainika kuwa rushwa ambayo ipo katika sekta ya Wabunifu wa majengo na ujenzi hapa nchini ndiyo inachangia kwa kiasi kikubwa sekta iyo kuzorota .
Hayo yamesemwa na naibu waziri wa ujenzi wa nyumba na makazi ya watu Godluck Ole medeye wakati alipokuwa akifungua mkutao wa wadau mbalimbali wabunifu wa majengo wa Tanzania na taasisi wabunifu wa majengo Afrika mashariki iliyokuwa ikifanyika katika ukumbi wa Cordor uliopo jijini hapa.
Alisema kuwa sekta ya hii imekuwa aiendelei kutokana na rushwa ambazo zinatembea ndani ya sekta hii.
Alibainisha kuwa iwapo sekta yoyote itakuwa ikiendeshwa kwa kutegemea rushwa basi sekta iyo hatakaa kuendelea na itakuwa kila siku inalalamika .
"naiwapo basi ikibainika mtu ametoa rushwa sehemu yeyote basi afikishwe sehemu husika mara moja na achukuliwe hatua zaharaka"alisema Medeye.
Alitoa wito kwa kwa wafanyakazi wa sekta hii kujiendeleza kielimu ili kuweza kuchukuwa nafasi ya wakandarasi na wabuni wa nyumba ambao wameingia wengi hapa nchini.
Alisema kuwa kwa pia wajijengee tabia ya kuanzisha semina kama hizi ambazo zifanyike mara kwa mara ili waweze kukutana na kujadili changamoto mbalimbali ambazo wanakutana nazo katika kazi zao.
Aidha alisema kuwa kwakuwa watalaamu wa fani hii ni wachache basi waanzishe mfumo wa kuwasomesha wanafunzi wanaopenda kuwa wabunifu wamajenge pindi pale watakapo fika kidato cha sita na wakitaka kuendelea.
"mnatakiwa mjitoe kuwasomesha wanafunzi ambao wanafika kidato cha sita na wanapenda kusomea fani hii ya ubunifu wa majengo pia muanzishe zawadi za mara kwamara ambazo mtatoa kwa wanafunzi ambao watafaulu vyema katika masomo yao ya kozi hii ya ubunifu wa majumba 'alisema Ole medeye
Alisema kuwa kwa sasa ivi hamna haja ya kuingia ubia kwa sababu sisi wenyewe tunamapungufu bali kitu kinachotakiwa ni kujiwezesha kwanza wenyewe kwa kwenda kuongeza elimu ili waweze kuwadhibiti watu hawa ambao wanakuja kufanya kazi hizi hapa nchini.
kwa upande wa rais wa chama cha wabunifuu wa majengo Tanzania Mbaraka Igangula Alisema kuwa changamoto kubwa ambayo inawakabili ni kukosa fedha za kujiendeleza na kufanya kazi kwani serekali pamoja na hasasi za mikopo hawawapi ushirikiano kama watu wanje wanavyotoa ushirikiano kwa wabunifu wa majengo .
Alisema kuwa wamekuwa wanashindwa kufanya kazi kutokana na kunyimwa fedha za mikopo ambazo wanaenda kuomba katika hasasi mbalimbali za mikopo .
''Sasa unaenda kuomba ela katika hasasi wakukopeshe wanakunyima wakati hawa wenzetu wanapewa ushirikiano wanakopeshwa katika nchi zao na wanakuja huku kufanya vitu bila ela kweli unaweza fanya kitu "alisema Igangula
Alitoa wito kwa serekali pamoja na asasi hizi za mikopo kuwa na utayari wa kuwawezesha kwa kuwapa mikopo ili waweze kazi na serekali iwaangalie sana wabunifu wa majengo wa hapa nchini na sio kukimbilia wabunifu kutoka nje ya nchi.