katika uzinduzi huu wa filamu hii ya fijana wa Arusha Shumileta naye alikuwepo apo akipata kinywaji
Mkurugenzi wa kampuni ya matangozo ya Mwandago ,Faustin Mwandago ambaye alikuwa mgeni rasmi wa uzinduzi huo aliyevaa suti akihutubia wasanii
Kikundi cha wasanii cha mjini hapa kijulikanacho kama Faiter kimezindia rasmi jana kanda yao ya kwanza ijulikanayo kama The killer katika ukumbi wa Active ulioko jijini hapo.
Akizindua kanda hiyo mgeni rasmi ambaye ni mkurugenzi wa kampuni ya Mwandago Investimenti Faustin Mwandago alisema kuwa amefurahishwa sana na kikundi hicho ambacho ni cha vijana kutoka Arusha kukaa chini na kufikiria kitu cha kufanya.
Aliwapongeza kwa jinsi walivyojituma mpamka wakafikia hatua ya kuzindua filamu hiyo ambayo alisema kuwa kwa kuwaangalia hakutegemea kama kuna vijana wa mkoani hapa wenyevipaji vya namna hile.
Alisema kuwa yeye kama mwandago atawasaidia vijana hao kuwajengea ofisi kwa ajili ya kukutana na kujifunza .
Alisema kuw a kikundi hichi kinasaida pia kuwaondoa vijana wengi wanaozurura mtaani kwani kinawapatia ajira moja wapo ivyo ata kuwa tayari kuwasaidia kwa kitu chochote.
Katika uzinduzi huu wa filamu pia uliuthuriwa na wasanii mbalimbali akiwemo shumileta ambapo yaye aliwapongeza vijana hawa kwa jinsi walivyotengeneza filamu hiyo na pia aliwapa wito akisema kuwa ni vyema wameamua kingia kwenye sanaa na kusema kuwa wakaze buti wasione kuwa wamefika.
“sasa ivi mnatakiwa mkazane sana mkaze buti kilamtu anatakiwa afanye aonyeshe kipaji chake na asijisikie akaona ndo amefika huu ni mwanzo wanatakiwa mjitaidi huu ni mwanzo msipende kujisia fanyeni kazi ionekana msifiwe na watu huo ndo usanii “alisema shumileta..
Alitoa wito kwa sanii ambao ndo wameingia kwenye fani kujitaidi sana kudumisha utamaduni wetu na kutopenda kuiga mambo ya nje kwani hata watu wa nje wanadumisha na kutangaza utamaduni wao ivyo watumie nafasi hiyo ya usanii kudumisha utamaduni woa.
Kikundi hichi cha faiter kiko chini ya usimamizi wa msanii mkongwe wa filamu anayetambulika kwa jina la Bad Boys na aliamua kuanzisha kikundi hichi ili kuinua na kuona avipaji vya usanii vya vijana wa Arusha .
Pia kikundi hichi ndicho kiliweza kuwatoa wasanii wengi akiwemo Dogo janja ambaye kwa sasa anajitaidi sana katika game.