leo ni siku ambayo Chadema pamoja na ndugu wa marehemu na wananchi wa mkoa wa Arusha wanakutana katika viwanja vya NMC kuaga miili ya marehemu waliouwawa kwa risasi tarehe tano katika vurugu za wananchi wanaosadikiwa kuwa ni wafuasi wa chadema na polisi .
miilii hiyo ambayo itaagwa rasmi kuanzia saa nne ikiambatana na misa pamoja na harambee za kuwachangia ndugu za marehemu itahuthuriwa na viongozi mbalimbali wa chama cha demokrasia na maendeleo Chadema akiwemo Mwenyekiti wa chama hicho Freeman Mbowe,katibu mkuu wa chama hicho Dr.wilbord Slaa pamoja na mbunge wa jimbo la moshi mjini Ndesamburo na mbunge wa jimbo la Arusha mjini Godbless Lema na wengine wengi.
Kabla ya misa hiyo kuanza nilibahatika kuzungumza na baadhi ya wananchi wa jiji la Arusha kuhusiana na msiba huu nao walisema kuwa wamesikitishwa sana na msiba huu na wamesikitishwa sana na kitendo ambacho jeshi la polisi walikifanya cha kuwauha watu hawa ambao hawana hatia kwa risasi.
Walisema kuwa katika vurugu hizo hapakuwa na sababu yeyote ya kutumia silaha wangetakiwa watumie maji na mabomu kama walivyoanza mwanzo kwani kuchanganya kwa kwa silaha za moto ndo zimesababisha vifo hivi vyote.
Mara baada ya misa hiyo kufanyika pamoja na harambee hizi kufanyika pia chadema wamejipanga kutoa tamko lao rasmi leo kuhusiana na mahuaji hayo na pindi tu wakimaliza miili hii itapelekwa sihemu husika yaani kuzikwa na ya kusafirishwa itasafirishwa ,
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia