ANDENYENYA ANENA HUKU CHANGONJA AMSHANGAA ZITTO

Jeshi la polisi mkoani hapa limesema kuwa hawajafanya kosa kuvuruga mkutano na maandamano ya chadema kwani yalikuwa yanatarajiwa kuleta mathara makubwa zaidi ya yaliyotokea.

Hayo yamesemwa na kamanda wa polisi wa mkoa wa Arusha Thobias Andengenye wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari ofisi kwake kuhusiana na vurugu zilizotokea mkoani hapa.

Alisema kuwa jeshi lao limetenda haki kabisa kuvuruga maandamano hayo na mkutano huo kwani iwapo vingefanyika kungeweza kutokea mathara makubwa zaidi ambayo yangewapata wananchi pamoja na malizao.

Alisema kuwa mpaka sasa vurugu hizo zimeweza kuleta mathara kwani idadi ya watu wanaoa kufa kutokana na vurugu hizo zimeongezeka kwani hivi leo ameongezeka mtu mmoja ambaye hali yake aikuwa nzuri na kusababisha idadi ya watu waliokufa katika vurugu hizo kufikia watatu.

Alimtaja mtu huyo kuwa ni Ismail Omari (37) mkazi wa Ungalimited ambaye yeye alijeruliwa kwa risasi tumboni katika fujo hizo na kusisitiza kuwa amefariki leo asubuhi(Jana) katika hospitali ya mkoa ya Mounti Meru na mwili wake umeifadhiwa katika chumba cha kuifadhia maiti cha hospitali hiyo.


Alisema kuwa wao kama jeshi la polisi hawawezi kusema kuwa watafanya chochote kwa watu hawa ambao wamefariki katika vurugu hizi bali wataangalia kama wataweza kuuthuria katika mazishi kama watu wengine wanavyo uthuria.

"sisi kama polisi atuwezi sema tunahuthuria katika mazishi haya ya hawa watu wala kuwalipa bali tutaangalia kama tutaweza kuzika kama watu wengine wanavyoenda labda amri itoke juu"alisema Andengenye

Kwa upande wake Kamishina wa Operesheni na mafunzo ya jeshi la polisi Paul Changonja aliwaambia waandishi wa habari kuwa wamewatoa viongozi wa chadema walikuwa ndani kwa kufuata utaratibu kanuni na sheria na sio kwa kufuata shinikizo la Zitto.

Alisema kuwa anamshaanga sana Zitto Kabwe kwa kitendo cha kutoa amri viongozi wa chadema watolewe na kutopewa mashariti yeyote kitu ambacho hakutegemea kabisa mtu kama yeye angeweza kuongea.

"namshangaa sana zito kuzungumza maneno kama haya anazungumza maneno bila ya kufikiria kweli na wakati chadema ndowamesababisha haya yote wasilikwepe hili na wala wasitafute njia ya kulikwepa kabisa "alisema Changonja

Alimalizia kwa kuwapa pole wale wote waliopata mazara na kusema kuwa kwa sasa wasiwe na wasiwasi kwani hali ya mji wa arusha imerudi sehemu yake na kutakuwa na fujo tena

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

Previous Post Next Post