BREAKING NEWS

Wednesday, January 12, 2011

WATATU WAAGWA JANA

Imebainika rasmi kuwa watu watatu wamekufa katika vurugu zilizotokea jana baada ya Polisi kutumia nguvu kwa kuwapiga mabomu na risasi za moto, wafuasi wa chama cha Chadema.

Habari za fifo hivyo limethibitishwa na polisi pamoja na hospitali ya Mkoa ya Mt Meru kupitia Mganga Mkuu wa Hospitali hiyo ambapo pia watu 26 vbado wamelazwa kutokana na kujeruhiwa vibaya kwa risasi na mawe.
Wakati idadi hiyo ya watu watatu kuthibitishwa na Mganga Mkuu wa Hospitali hiyo,Dr Salash Toure Kamanda wa jeshi la Polisi, Thobias Andengenye alisema waliokufa ni wawili

Marehemu hao waliofariki katika vurugu hizo wametajwa na Kamanda wa Jeshi la Polisi Thobias Andengenye kuwa ni George Mwita Mwaitara, ni mtu mzima na mwingine hakupata jina lake.

Pia Majeruhi waliojeruhiwa amewataka kuwa ni Josephine Slaa, Richard Mtui, ambaye ni Katibu wa Mbunge wa Hai, Charles Ole Msaki, Juma Samweli Wambura, Kennedy Bundara, Ally Nehemia na Polisi watatu ambao hakuwa tayari kuwataja majina yao, ambao nao wamelazwa katika hospitali ambayo pia alificha kuisema.

Akizungumzia tukio hilo Kamanda wa Polisi Mkoani Arusha, Thobias Andengenye, alisema kuwa tukio hilo lilitokea jana Desemba 5 mwaka huu, majira ya saa 6.00 mchana, kwenye eneo la Tenki la Maji na baadaye viwanja vya NMC ambako walifanya mkutano wa hadhara.

Alisema kuw abaada ya kukusanyika katika eneo hilo bila kibari cha Polisi, ndipo Polisi walipolazimika kutumia nguvu na kuwatia mbaroni watu 49, wakiwemo, viongozi wa ngazi ya Kitaifa Chadema.


Alisema kuwa pia sababu ya kuwakamata ni pale Viongozi wa ngazi za juu za chama hicho kuhamasisha wananchi kuvamia kituo cha Polisi kufanya vurugu kw alengo la kuwatoa Mahabusu ambao ni viongozi wao.

Aliwataja viongozi waliowekwa rumande kuwa ni Wilbroad Slaa, Freeman Mbowe, Phillimon Ndesamburo, Joseph Selathini, Basil Lema ambaye ni Katibu wa itifaki Chadema Taifa.

Kamanda Andengenye alisema kuwa, baada ya kuwatia mbaroni washitakiwa hao, wafuasi wa chama hicho walianza kuwarushia mawe Polisi na wakati polisi wakitumia mabomu na risasi za baridi, ndipo wafuasi hao walipovamia jengo la mfanyabiashara mmoja, Salmu Ally, eneo la Metro Pole na kuteketeza kwa moto, ambapo mali zilizoharibika hazijajulikana.

Pia alitaja uharibifu mwingine uliofanyika ni kuchoma moto kibanda cha Arusha Annex By Night, ambao polisi kwa ushirikiano na kikosi cha zima moto, waliwahi kuzima moto huo kabla ya kuunguza majengo ya jirani.


Kamanda huyo alisema kuwa wafuasi hao waliendelea na mashambulizi yao na kuvamia kituo cha Polisi cha Unga limited na Kaloleni na kumwaga mafuta ya Petroli kw alengo la kuchoma moto, ila kwa bahati Polisi waliwahi kuwasambaratisha.

Alisema kuwa kwa tukio lililotokea, ndiyo maana tangu mwanzo walizuia maandamano hayo, kwa sababu walipata taarifa za usalama kuwa kuna vijana wamepanga kufanya uharibifu wa mali na ndicho kilichotokea.

Hata hivyo alisema washitakiwa wote watafikishwa Mahakamani kusomewa mashitaka yao ya kufanya maandamano bila kibari.


Kwa upande wa kamishina wa Operesheni wa Jeshi hilo, Paul Chagonja, alipowasili kwenye ofisi za Kamnada wa jeshi la Polisi, Mkoani Arusha, aliwaomba msamaha waandishi w ahabari waliuopigw ana kupata usumbufu wowote, na kudai kuwa haikuwa nia yao, isipokuw akwenye vurugu hawawezi kujua nani ni nani.

Share this:

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

 
Back To Top
Copyright © 2014 MOUNT KILI NEWS. Designed by OddThemes | Distributed By Gooyaabi Templates