MWAKILISHI WA UBALOZI AFRIKA KUSINI AWASILISHA HATI YA UTAMBULISHO

MWAKILISHI wa Ubalozi wa Afrika Kusini nchini jana...
MWAKILISHI wa Ubalozi wa Afrika Kusini nchini jana aliwasilisha hati za utambulisho kwa Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki barozi Juma Mwapachu.


Balozi Mwapachu alisema hati hizo zitasaidia kuimarisha ushirikiano miongoni mwa wanachama wa jumuiya hiyo,hasa katika kupata taarifa sahihi za kimaendeleo.


“Hii inatoa fursa kwetu kuangalia umuhimu wa mtangamano wa kikanda barani Afrika, katika wakati huu muhimu wa kupongeza mafanikio yaliyopatikana katika jumuiya yetu,” alisema Mwapachu.


Alifafanua kuwa msukosuko wa kiuchumi duniani umeonyesha umuhimu wan chi kufanyakazi pamoja ili kuimarisha mahusiano ya kibishara baina ya kanda na bara la Afrika kwa ujumla.


Alisema uhusiano huo wa kibiashara unachangia kwa kiasi kikubwa uchumi na maendeleo ya kikanda.


Mwapachu alibainisha kuwa ushirikiano wa SADC, COMESA na EAC una umuhimu mkubwa katika kukuza uchumi katika kanda ya Afrika Mashariki na kati.
Alisema Afrika Kusini ni mshirika mzuri katika kukuza ushirikiano wa kibishara barani Afrika na kanda zake zote.


Alisema katika kujenga miundombinu imara inayoendana na matakwa yaliyoainishwa kwenye NEPAD.


Tayari nchi 16 kutoka nchi mbalimbali duniani na mashirika ya kimataifa zimeteua wawakilishi wao kwenye jumuiya ya Afrika Mashariki.

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

Previous Post Next Post