BREAKING NEWS

Tuesday, January 25, 2011

Wanafunzi wa mwaka wa kwanza wa chuo kishirikishi cha Tumaini(Makumira Universty) jana wamegoma kuingia madarasani na kuandamana hadi katikati ya barabara kuu ya Arusha moshi na kuziba barabara kwa kuweka mawe njiani na kuzuia magari kupita hali iliyosababisha askari wa jeshi la polisi kuwatawanya kwa mabomu ya machozi.

wanafunzi hao ambao walikuwa wamebeba mabango yenye ujumbe tofuti walidai kuwa chanzo cha maandamano hayo ni kufikiasha ujumbe kwa wananchi kwa wananachi na serekali kuhusiana na mikopo yao kucheleweshwa hali inayowafanya kuishi katika mazingira magumu sana.

Wakiongea kwa wanafunzi hao kwa hasira walisema kuwa ni mda mrefu sana wamekaa wakisubiri kutumiwa mikopo yao lakini ailetwi na wamepeleka malalamiko katika bodi ya mikopo lakini hayafanyiwi kazi na hadi sasa wanakaa kwa tabu sana kwani wakati mungine wanakosa hata ela ya kula chuoni hapo.


Walidai kuwa cha kushangaza zaidi hata uongozi wa chuo hicho hauwasaidii kwakitu chochote wamewapelekea malalamiko wanayapuuzia na kitu kilichowauma zaidi mpaka kikawafanya waandamane ni kitendo cha mwenzao kuumwa gafla kutokana na kupata mshituko baada ya kukuta jina lake alipo katika orotha ya wanafunzi ambao wanatakiwa kupewa mikopo huku mwanafunzi huyo akiwa ni yatima.

"kwa upande wa shule hawajatusaidia chochote mara baada ya kuona mwenzetu salome ameanguka badala yake wamegoma ata kutoa hela ya kumtibu hospitali na wanatufata sisi wanatuambia tuchange shilingi laki moja kwa ajili ya kumuudumia mwenzetu tukirudi nyuma sisi hapa atuna hata shilingi mia ya kula"walisema wanafunzi hao.

Mwanafunzi mwingine ambaye alijitambulisha kwa jina la Jackilini Mzovia alisema kuwa yeye anasikitishwa sana na bodi hii ya mikopo kwa kuwacheleweshea hela kwani inawafanya wao kuishi katika mazingira magumu kiasi kwamba kuna baadhi ya wanafunzi wenzao wameshidwa kuvumilia mpaka wamefika hatua ya kujiuza .

wameiomba serekali ifanye jitahada ya kuwasaidia wanafunzi hao mikopo ili waweze kujikwamua katika hali hiyo ya umaskini kwani wakilifumbia macho watapoteza vijana wengi ambao wanategemewa kuwa viongozi wa baadaye haswa ukiangalia kuna gonjwa hili hatari la Ukimwi.

kwa upande wa mwanafunzi mungine aliyejitambulisha kwa jina Kristiani Abati alisema kuwa wao wanawasisi na chuo kuwa kinaweza kikawa kimepokea fedha zao na kuzichakachua kwani hata walivyoitwa kusaini cheki ya mikopo ya watu hao 78 iliyokuja ilionyesha imetolewa tangu November 5 lakini cha kushangaza wamekuja kupewa January 21 mara baada ya wao kupiga kelele sana.

kwa upande wake mkuu wa chuo hicho Joseph Parsalaw alisema kuwa anashangazwa sana na hatua ambayo wamechukua wanafunzi hao kwa kufanya kitendo cha kuandamana na kufanya fujo kwani hakijawahi kutokea chuoni hapo na kama matatizo yao waliyasikia na walikuwa katika kikao wakiyajadili namna ya kuyatatua.

Alibainisha kuwa wao kama chuo hawazuii wala hawatoi mikopo kwa wanafunzi hao bali wanatumia serekali ya wanafunzi ambao inawasilisha wanafunzi hao katika bodi ya mikopo .

Alidai kuwa rais wa wanafunzi chuoni hapa alikwenda katika bodi ya mikopo ambapo alikuta jumla ya wanachuo 642 wameshapatiwa mikopo na 84 bado asilimia za mikopo yao haijulikana huku wengine 136 asilimia zao hazijaonekana katika bodi ya mikopo.

"mimi licha ya ivyo nashangaa sana kwani hapa chuoni kunawanachuo kama 2000 lakini navyojua niwanavyuo 47 tu ambao hawajapata mikopo yao lakini wengine wote tayari"alisema Parsalaw.

kwa upande wa hati ya malipo alisema kuwa chuo hakija chakachua hati hiyo kwani pamoja iliandikwa kuwa imetoka Novembar 5 lakini imewasilishwa chuoni hapo January 21 .

Alisema kuwa wanadhani kitu ambacho kimechangia ni mvuto wa nje umesaidia na kuchangia .

"wameona wanafunzi wenzao katika vyuo vikuu vingine wakiandamana wakidai mikopo yao sasa na wao naona wakaamua kufata mkumbo wakithani ndio njia sahihi ya kupata haki"alisema

Alimalizia kwa kusema kuwa chuo hakijahusika na tatizo la wanafunzi hao kucheleweshewa mikopo yao na amehaidi kuwa chuo kitaendelea kuwasilaiana na bodi ya mikopo ili kujua hatima ya mikopo hiyo ya wanafunzi hao.


Naye kamanda wa jeshi la polisi mkoani Arusha Thobiasi Andengenye amesema kuwa mpaka sasa jeshi hilo limewashikilia wanafunzi 21 kwa ajili ya mahojiano ya kubaini kwanini wameandamana na kwa kufanya fujo.

Alisema kuwa wao waliamua kuingilia kati kutokana na kuona wanafunzi hao wamezuia barabara kuu iendayo Arusha -moshi kwa muda wa saa moja na kusababisha msongamano mkubwa wa magari pamoja na kusababisha usumbufu kwa wananchi waishio maeneo hayo pamoja na magari ya pitayo katika barabara hiyo.

Andengenye alisema kuwa kama kweli wanafunzi hawa wanadai kwanini wasi kwanini wasifuate sheria husika badala ya kujichukulia hatua ya kufanya fujo.

Share this:

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

 
Back To Top
Copyright © 2014 MOUNT KILI NEWS. Designed by OddThemes | Distributed By Gooyaabi Templates