10 KWENDA MOROGORO OPEN

Wachezaji wa mchezo wa Gofu wa Klabu ya Arusha Gymkana wanatarajia kuondoka February 4 kuelekea mkoani Morogoro kushiriki mashindano ya mchezo wa gofu yajulikanayo kama Mororogo Open yanayotarajia kufanyika kwa muda wa siku mbili.

Akiongea kocha mkuu wa klabu ya Arusha gymkana Olasi Molel alisema kuwa haya ni mashindano ya kwanza ya mchezo wa gofu kufanyika kwa mwaka huu na mkoa wa morogoro ndio umebahatika kufuangua mashindano haya kwa mwaka huu.

Alsiema kuwa mashindano haya ni yawazi na yanatarajiwa kufanyika kwa muda wa siku mbili ikiwa ni Februal tano na sita na yanatarajiwa kufanyika katika klabu ya mchezo wa gofu ya morogoro.

Alisema kuwa mashindano haya ni ya wazi ivyo vilabu vyote vya mchezo wa gofu vinaruhusiwa kushiriki na wachezaji wa rika zote piawanaruhusiwa.

"haya ni mashindano ya wazi ivyo wachezaji wa rika zote wanaruhusiwa kushiriki na kucheza na pia klabu hii ya morogoro inabahati kwani haya ni mashindano ya kwanza kwa mwaka huu na yanafanyikia kwao"alisema Molel.

Alisema kwa klabu yao jumla ya wachezaji kumi wanaenda kushiriki mashindano hayo.

Aliwataja wachezaji wa klabu ya Arusha ambao wanaenda kushiriki mashindano haya kuwa ni Nuru molel,Julius Frances,John Said,Elisante Lemburis,Jimmi Molel,Ruth Chubirwa pamoja na Richardi Gomes.

Kwa upande wa wanawake alisema wapo Lina Frances ,Neema Olomi pamoja na Madina Iddi.

Molel alisema kuwa mashindnao haya ya wazi ya mchezo wa gofu wa morogoro yamethaminiwa na kago Stax ambao pia wamejitolea kuthamini mashindano yote ya wazi ya gofu yanayofanyika katika vilabu vyote

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

Previous Post Next Post