Twendeni sasa tukaone iyo mitambo yenyewe bwana wa kwanza kushoto ni kaka Devidi akiwa yupo kikazi zaidi anaongozana na waeshimiwa
Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Magesa Mulongo
(kulia), akisalimiana na viongozi wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL),
alipowasili katika hafla ya uzinduzi wa mtambo wa nne wa usafishaji maji
yaliyotumika kiwandani kuwa maji salama kwa matumizi ya binadamu
katika Kiwanda cha Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) cha Arusha, mwishoni
mwa wiki.Kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Ufundi wa TBL, Gavin van
Wijk, Meneja wa Kiwanda TBL Arusha,Bert Grobbelaar na Mkurugenzi
Mtendaji wa TBL, Robin Goetzsche. Wa pili kulia ni Waziri wa viwanda na
Biashara ,Dk. Cyril Chami.
Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Magesa Mulongo
(kulia), akifunua pazia kuonesha jiwe la msingi wakati wa uzinduzi wa
mtambo wa nne wa usafishaji maji yaliyotumika kiwandani kuwa maji
salama kwa matumizi ya binadamu katika hafla iliyofanyika katika
Kiwanda cha Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) cha Arusha, mwishoni mwa
wiki.Anayeshuhudia uzinduzi wa mtambo huo uliogharimu sh. bilioni 3.6,
ni Mkurugenzi Mtendaji wa TBL, Robin Goetzsche.
KIWANDA cha Bia nchini (TBL) kilichopo mkoani hapa kimezindua
mtambo maalumu wa kusafisha maji yatokanayo na shughuli za uzalishaji
kiwandani hapo.
Kuzinduliwa kwa mtambo huo kunatajwa kuwa hatua muhimu ya kuhifadhi
mazingira na maji ya Mto Themi unapita jirani na kiwanda hicho.
Meneja Mkuu wa TBL, Robin Goetzsche alisema uzinduzi wa mtambo huo
hapa mjini Arusha ni hatua muhimu kwa kiwanda kwa sababu itawasaidia
kutimiza dhamira yao ya kulinda mazingira.
“Mtambo huu utakuwa na uwezo wa kusafisha asilimia 60 ya maji machafu
yatokanayo na shughuli za uzalishaji kiwandani. Uongozi wa kampuni hii
itaendelea kuwekeza katika kuleta teknolojia bora itakayotusaidia
kuhakikisha uzalishaji wetu unakuwa salama kwa mazingira na kwa binadamu
pia,” alisema.
Naye Meneja wa Kiwanda hicho, Bert Grobbler akizungumzia mtambo huo
alisema, una uwezo wa kusafisha maji kiasi cha hektolita 12,720 sawa na
lita 1,272,000 kwa siku zenye wastani wa uchafu tani 3.8 kwa siku.
“Maji kutoka kiwandani huchujwa taka ngumu kama vipande vya chupa,
lebo, machicha na vitu vingine, baada ya hapo huingizwa kwenye tangi la
kwanza kwa ajili ya kuchanganywa kabla ya kuingizwa kwenye tangi lenye
wadudu wasiotumia hewa ya oksijeni ambao hao ndio huondoa na kupunguza
uchafu kwa asilimia 85.
“Mchakato huo huendelea kwa kupitisha maji kwenye matangi mengine
yenye wadudu watumiao hewa ya oksijeni napo pia hupunguza uchafu
uliobaki kabla ya kupitisha kwenye tangi la mwisho la kuchuja ili
yamwagwe kwenye vyanzo vya maji bila kuathiri mazingira,” alisema
Grobbler.
Alisema mtambo huo hufanikisha kumwaga maji yenye kuzingatia viwango
vya utunzaji mazingira na Shirika la Ubora wa Viwango (TBS) vya Tanzania
kwa kitaalamu.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Magesa Mulongo akizungumza
katika uzinduzi huo aliipongeza TBL kwa kuwa mstari wa mbele katika
kukabiliana na changamoto za uchafuzi wa mazingira.
“Nchi nyingi zinazoendelea kwa viwanda duniani zimekuwa zikikabiliwa
na uchafuzi wa mazingira ni rai yangu kwa wamiliki wa viwanda mkoani
kwetu na asasi zinazojishughulisha na utunzaji wa mazingira
zitashirikiana kuhakikisha jiji na makazi yake yanakuwa safi na salama
muda wote,” alisema Mulongo.