BREAKING NEWS

Monday, March 18, 2013

MGOMO WA DALADALA WATIKISA ARUSHA LEO








Mkoa wa Arusha umekubwa na mgomo wa daladala ambao umepelekea maelfu wa wananchi wanaoishi katika jiji hilo kulazimika kutembea kwa miguu umbali mrefu kuelekea makazini hali iliyosababisha shughuli za kiuchumi  kusimama kwa muda mrefu.


Hali hiyo imedhirika mjini hapa ambapo shughuli nyingi zimechelewa kuanza ikiwemo biashara  ya maduka na masoko ya bidhaa  mbalimbali kutokana na wahusika kukosa usafiri wa kufika katika maeneo yao ya kazi,ambapo licha ya shughuli za uchumi wanafunzi wengi ambao mpaka majira ya saa 5 asubuhi walikuwa bado hawajafika mashuleni na wengine kushindwa kufika kabisa


Kila kona ya mji wa Arusha hapakuwa na daladala iliyoonekana ikifanya safari zake,ambapo madereva na makondakta walisimama karibu kila barabara ya jiji la Arusha na  viunga vyake wakihakikisha kuwa hakuna daladala inayosafirisha abirikia.


Juma Omari na Issa Ramadhani am,bao ni madereva wa daladala mkoani Arusha wanaeleza kuwa wameamua kufanya mgomo huo ili kushinikiza madai yao ikiwemo kuwepo kwa vituo rasmi vya kupanda haice na kushushia abiria kwani  hakuna vituo rasmi na wamekuwa wakikamatwa na kupigwa faini kuanzia shilingi laki moja na nusu 150,000 hadi laki tatu 300,000 jambo linalowaathiri katika biashara zao.


Kwa upande wake Mkuu wa WIlaya ya Arusha  John Mongela akizungumzia mgomo huo amekiri kuwa rushwa kwa polisi wa vikosi vya usalama wa barabarani ni tatizo sugu na tayari wamekutana na wadau wa usafirishaji ili kulitafutia ufumbuzi suala hilo,ikiwa ni pamoja na suala la  vituo ambapo amesema kuwa wako katika mkakati wa kukaa na wataalamu kuainisha maeneo maalumu ya vituo.

Share this:

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

 
Back To Top
Copyright © 2014 MOUNT KILI NEWS. Designed by OddThemes | Distributed By Gooyaabi Templates