MKAZI
wa Kijiji cha Kibrash Wilayani Kilindi Mkoani Tanga,Abdalah Kisailo (58)
amehukumiwa kwenda jela kifungo cha miaka 15 na faini ya sh5 milioni kwa kosa
la kukutwa kwenye hifadhi ya Taifa ya Tarangire akitaka kufanya ujangili.
Kisailo
alihukumiwa juzi kwenye Mahakama ya Wilaya ya Babati Mkoani Manyara,mbele ya
Hakimu Mfawidhi wa Mahakama hiyo Victor Bigambo kwa kosa la kujiandaa kuwinda
tembo na kukutwa na bunduki mbili zenye risasi.
Awali,Mwendesha
mashtaka wa kesi hiyo,Linus Bugaba alisema Kisailo alitenda kosa hilo Octoba 17
mwaka jana saa 10 jioni,kwenye hifadhi ya Tarangire katika eneo la Kijungu
wilayani Kiteto mkoani Manyara.
Bugaba
alisema Kisailo alikamatwa na mhifadhi Richard Shilungi akiwa na silaha aina ya
bunduki mbili aina ya Rifle 425 yenye namba ya ZA 52602202 na Rifle 375 yenye
namba 42979 na risasi kumi na risasi 15 za kienyeji.
Alisema
pia mshatakiwa huyo alikamatwa akiwa na shoka moja na dumu moja la maji hivyo
aliiomba mahakama hiyo imepe adhabu kubwa mshtakiwa huyo ili iwe fundisho kwa
watu wengine wenye tabia ya kufanya ujangili katika hifadhi.
Hata
hivyo,Hakimu Bigambo alikubaliana na ombi hilo na akamuhukumu Kisailo kwenda
jela miaka 15 na pia alipe faini ya sh5 milioni kwa makosa mawili ya kumiliki
bunduki mbili bila halali na kutaka kufanya ujangili hifadhini.
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia