Ndugu
Mwenyekiti wa Umoja wa Wakuu wa shule za sekondari Tanzania[TAHOSSA] wilayani
Hai,
·
Ndugu
Viongozi wa TAHOSSA,
·
Ndugu
Afisa Elimu wa wilaya,
·
Wakuu
wote wa Shule za sekondari wilayani Hai.
Awali ya yote nianze kwa kumshukuru mwenyezi Mungu kwa kutupa uzima na
kutukutanisha hapa leo lakini pili kutuwezesha kuendelea na kazi katika mwaka mpya wa 2013.
Kwa wale ambao hatujakutana pamoja na kwamba huu ni mwezi Machi lakini
kuna msemo wa kiingereza “Late better
than never”,hivyo basi nitumie
fursa hii kuwatakia mwaka mpya mwema wenye upendo na uwajibikaji.
Lakini jambo la pili nichukuwe fursa hii kuwashukuru
kwa kunialika kuzungumza machache kwenye Mkutano huu na niwapongeze waandaaji kwa kuweza
kuwakutanisha wakuu wa shule za sekondari katika wilaya ya Hai.
Ingawa ni jumuiko la kawaida kwa kila mwaka lakini
kupata idadi kubwa ni mafanikio makubwa hongereni sana.
Ndugu Mwenyekiti, Mkutano huu unafanyika katika
kipindi hiki ambacho mjadala mkubwa hapa nchini ni matokeo ya kidato cha
nne.Lakini Matokeo hayo ni hitimisho tu ya matokeo mengine ya darasa la saba na
yale ya kidato cha pili.
Mnamo tarehe 18 Februari, 2013 Baraza la Mitihani la
Taifa lilitangaza matokeo ya Mtihani wa Taifa wa Kidato cha Nne ya mwaka
2012. Wanafunzi 397,132 walifanya mtihani huo na kati ya hao, waliofaulu
ni 126,851 yaani sawa na asilimia 34.5. Wanafunzi 240,903 ambao ni sawa
na asilimia 65.5 hawakufaulu mtihani huo.
Matokeo ya mitihani ya huo, yameshtua na kufadhaisha
watu wengi nchini kwani hata shule zinazofahamika kuwa na historia ya
kufaulisha vizuri kama vile seminari, shule za watu binafsi, za mashirika ya
dini na sekondari kongwe za Serikali ambazo hazina matatizo kama ilivyo kwa
zile sekondari za Kata, nazo safari hii hazikupata mafanikio kama ilivyo
kawaida yao
Kwa upande wa wilaya ya Hai katika shule za serikali
watahiniwa 1,688 wamefeli kabisa kwa kupata sifuri.Kwa upande wa
ufaulu,wanafunzi wawili walifanikiwa kupata daraja la kwanza,wanafunzi watano
daraja la pili,wanafunzi 44 daraja la tatu na wanafnzi 555 daraja la nne.
Kwa upande wa shule za binafsi,wao wamepata daraja
la kwanza wanafunz 11,daraja la pili wanafunzi 44,daraja la tatu wanafunzi 111
na daraja la nne wanafunzi 405 ilhali waliofeli ni wanafunzi 145.
Kwa upande wa kidato cha pili ni vivyo hivyo,Wilaya
ya Hai imefanya vibaya kwa kupata
wastani wa ufaulu wa asilimia 35 huku kiasi cha wanafunzi 940 wanalazimika
kubakia katika kidato cha pili wakiwa miongoni mwa wanafunzi 2,959 walifanya mtihani huo.
Ndugu mwenyekiti,Nyinyi mliopo hapa ni wadau nambari
moja wa elimu katika wilaya yetu ya Hai na bahati nzuri mmekutana wakati hivi sasa kila mmoja wetu yuko katika
kuangalia tunafanya nini kuinusuru elimu yetu.
Uongozi wa serikali katika wilaya umeshapanga kuwa
na mkutano na wadau wa elimukuzungumzia mikakati inayolenga kuinua hali ya
elimu na kukomesha kabisa dosari zote ambazo zinasababisha elimu yetu kwenda
chini ama kuzorota.
Ndugu mwenyekiti,mwezi uliopita nilikuwa na kundi la
wanafunzi wa vyuo vikuu mbalimbali wanaotoka wilaya ya Hai kupitia Umoja wa
wanafunzi wanaosoma vyuo vikuu kutoka wilayani Hai[HAUSO] niliwaomba kwa kuwa
wapo likizo basi wajitolee kufanyakazi za kuwafundisha wadogo zao walioko
katika sekondari mbalimbali,hivyo walikubali na vijana kumi na tano walikuwa huko katika shule.
Lakini mbali ya kufundisha niliwaomba wanafanyiye
tathimini ya nini tunaweza kufanya katika kuhakikisha kuwa tunainua hali ya
elimu katika wilaya yetu ya Hai.
Kwa sasa wote wamesharejea vyuoni lakini nilibahati
kukaa nao na wamenieleza mengi ambayo wamyabaini katika shule zetu za sekondari
na katika kuyashughulikia nimeona baadhi ni ya kuchukulia mkakati wa muda mfupi
ama wa haraka.
Hivi sasa kuna vijana wetu ambao wana miezi michache
sana kabla ya kuingia katika mitihani ya kumaliza elimu ya msingi na huu ukiwa
ni mwezi machi na niliwauliza hao vijana vipi hali ipoje ? Nao walinijibu
kwamba tusipochukuwa hatua matokeo ya kidato cha nne kwa mwaka huu yanaweza
kuwa mabaya maradufu ya matokeo ya mwaka jana.
Hivyo nyinyi mkiwa wakuu wa shule kwa taratibu za halali
kabisa tuunganishe nguvu zetu katika kuchukuwa hatua za muda mfupi ambazo
zitawasaidia vijana ambao wanajiandaa kufany mitihani ya kumaliza kidato cha
nne wanafanya vizuri.
Kuna baadhi ya maeneo ambayo waliyaona na mengine
pia yamo katika taarifa mbalimbali za wakaguzi wa elimu zinazofanyika kwa
nyakati tofauti ambapo sisi kama wakuu wa shule tunaweza kujadiliana hapa na
kuweka mkakati wa kuchukuwa hatua kwa lengo la kuwasaidia vijana wetu katika
kujenga maisha.
Baadhi
waliyoyaona vijana wetu wa vyuo vikuu ni pamoja na;
1. Migogoro ndani ya ofisi za
shule yaani Staff Room.
Katika mwezi mmoja wa kufanya kazi wamebaini kwamba
katika baadhi ya shule kuna maelewano madogo ama hakuna kabisa kati ya mkuu wa
shule na makamu mkuu wa shule pamoja na mwalimu wa taaluma.
2. Nidhamu ya mavazi kwa baadhi
ya walimu.
Baadhi ya walimu wameondoka kabisa katika mazoea
ambayo tuliyajenga miaka ya nyuma kwa katika jamii zetu walimu ni mfano wa
kuigwa kwa kuingia katika mavazi yasiyokuwa ya staa yakiwemo ya kushusha
suruali chini maarufu kama kata K na kuteremsha sketi chini.
3. Mtihani wa Mock kutokuwa na
mfumo wa kuupima.
Mtihani huu haufanyiwi tathimini nzuri katika ngazi
ya wilaya ili uweze kutumika katika kuwaandaa watahiniwa wanaotarajiwa kufanya
mitihani ya kitaifa baada ya miezi michache mbeleni
4. Wanafunzi kushindwa kuelewa
Lugha ya kufundishia.
Bado kuna tatizo kubwa kwa idadi kubwa ya wanafunzi
wanaoanza kidato cha kwanza kuelewa vizuri lugha ya kujifunzia ya kiingereza
kutokana na kutumia lugha ya Kiswahili kwa muda ya miaka saba katika shule za
msingi.
5. Wanafunzi kuingia katika
mahusiano ya Kimapenzi.
Imebainika kuwa baadhi ya wanafuni wanaingia katika
uhusiano wa kimapenzi na hivyo kushindwa kujikitia katika masomo.
6. Wazazi kushindwa kutoa
ushirikiano kwa walimu.
Baadhi ya wazazi wamekuwa na tabia ya kwenda shule
kugombana na walimu mara walimu wanapochukuwa hatua za kuwarekebisha wanafunzi
wanaopooka.
7. Baadhi ya mada za masomo
hazifundishwi kabisa.
Imebainika kwamba baadhi ya topic katika masomo na
hasa hisababti pamoja na masomo ya sayansi hazifundishwi kabisa mpaka wanafunzi
wanamaliza elimu ya msingi
8. Kuingia kwa utandawazi na
teknolojia ya kisasa.
Baadhi ya wanafunzi kutumia vibaya teknolojia ya
kisasa hususani simu za mikononi na hivyo kujikita zaidi huko huku wakisahau
jukumu lao kubwa ambalo ni kujifunza na kuelewa kile wanachojifunza.
Vijana hao
walitoa baadhi ya mapendekezo yakiwemo ya mkakati wa muda mfupi wa kuwasaidia
vijana wetu ambao wanatarajia kufanya mitihani yao mwaka huu ambayo ni pamoja
na;
1. Kuwepo na utaratibu wa
kubadilishana kufundisha baadhi ya
Topic miongoni mwa walimu kwa walimu wa shule za
jirani kwa maana wa shule moja kwenda shule nyingine kutegemeana na umahiri
wake katika topic husika.
2. Kuongeza saa za kuwafundisha
kidato cha nne.
Wanafunzi wote wanaotarajia kufanya mitihani ya
kidato cha nne waweze kuwahi kufika shuleni saa moja asubuhi na baadaye warudi
tena jioni baada ya kutoka shule saa nane na nusu mchana
3. Kuandaliwa kisaikolojia.
Kutokana na matokeo ya mitihani iliyopita kuwa
mabaya basi kwa vyovyote vile hali hiyo inaweza kuwaathiri baadhi ya watahiniwa
watarajiwa na hivyo ni vyema ukaandaliwa mfumo wa kuwajenga kisaikolojia.
4. Mkazo katika kufundishwa
mbinu za kufanya mitihani.
Ratiba ya kufundishwa jinsi ya mbinu za kufanya
mitihani imekuwa fupi na hivyo ni vyema walimu katika shule wakaangalia mkakati
wa kuwafundisha wanafunzi mbinu za kufanya mitihani
5. Uimarisha wa bodi za shule.
Kuimarisha ama kufufua bdi za shule baada ya
kubainika kwamba shule nyingi katika wilaya ya Hai hazina kabisa bodi za shule
ama zilizopo zinashindwa kuwajibika.Kuwepo kwa bodi hizo kutaimarisha mahusiano
kati walimu na wazazi na kuweka mkakati wa pamoja na kuwasaidia wanafunzi.
6. Mpango wa kuwapa motisha
walimu wanaofanya vizuri.
Kwa walimu ambao watafanikiwa kuwezesha idadi kubwa
ya wanafunzi kufanya vizuri kwa kupata alama za juu za A ama B,basi kuwe na
utaratibu wa kuwazawadia na kutambua mchango wao katika elimu.
Ndugu mwenyekiti,Haya ni baadhi tu ya mapendekezo ya
muda mfupi ambayo nyinyi kama wana taaluma na wadau namba moja mnaweza
kuyajadili na kuyatengenezea mapendekezo kwa ajili ya kuchukuwa hatua katika
muda muafaka.
Mapendekezo mengine ni ya muda wa kati na mrefu
ambayo tutayatengezea utaratibu baada ya kumaliza mchakato wa kukutana na wadau
pamoja na makundi mbalimbali ambayo kwa namna moja yanahusika katika masuala ya
elimu.
Wilaya inawategemea sana katika kuirejesha katika
hadhi ya miaka ya nyuma kama miongoni mwa wilaya ambazo zilikuwa na wasomi
katika miaka ya awali mara tua baada ya uhuru mwaka 1961
Ndugu mwenyekiti baada ya masuala ya elimu ambayo
hasa ndiyo jukumu lenu kubwa kama wakuu wa shule za sekondari,naomba mniruhusu
kuongelea baadhi ya masuala ya kijamii kutokana na nyinyi mbali ya kuwa wakuu
wa shule lakini pia ni sehemu ya jamii na pia wengi wenu katika jamii mnanafasi
kubwa ya kukubaliwa na kuheshimika sana.
1.
Kukithiri kwa tabia ya
unywaji wa pombe ikiwemo pombe haramu ya gongo
Ndugu Mwenyekiti,sote tunafahamu vijana tunaowafundisha ni sehemu ya kundi kubwa la vijana katika wilaya yetu ambalo sasa hivi linaendelea kuangamia kutokana na kukithiri kwa unywaji wa pombe ikiwemo pombe haramu ya gongo.
Kwa mwananchi yeyote mwenye uchungu na wilaya yetu ya Hai lazima suala hili litamgusa kwani hivi sasa ni janga la wilaya na hali hii ikiendelea baada ya miaka mitano mpaka kumi ijayo hatutakuwa tena na kizazi kilichoandaliwa vyema kupambana na changamoto za maisha.
Lakini baya zaidi baadhi ya viongozi wenzetu katika vijiji na vitongoji wamekuwa vinara katika kuhakikisha biashara hii ya pombe haramu ya gongo inaendelea kudumu.
Rai yangu kwenu ni kushirikiana katika kuhakikisha kwamba tunaweka mkakati wa kupambana na watengenezaji,wauzaji na watumiaji wa pombe haramu ya gongo na kuhakikisha imekwisha kabisa.
Lakini mbali na pombe haramu ya gongo lakni kuna tatizo kubwa la matumizi ya pombe halali kwa muda kwa idadi kubwa ya vijana zikiwemo zile zinazobebeka kirahisi ndani ya mifuko ya plastki pamoja na pombe yetu ya asli ya mbege.
Pamoja na kuwepo kwa sheria ambayo hivi sasa
tumeanza kuitekeleza kwa nguvu zote lakini nyinyi kwa upande wenu naomba
niwaombe kwa nafasi zenu kuendelea kuelimisha jamii athari za kunywa pombe kwa
saa ishirini na nne ndani ya siku saba za wiki katika siku thelathini za mwezi.
Sisi kwa upande wetu tutaendelea kusimamia sheria ya
saa za unywaji wa pombe ambapo ni saa tisa jioni mpaka saa tatu usiku kwa siku
za katikati ya wiki na saa nne kwa mwisho wa wiki kwa maana jumamosi na
jumapili.
2.
Utunzaji wa mazingira
Ndugu Mwenyekiti,mazingira ndiyo uhai wetu.Kwa kutambua hilo na kasi kubwa iliyojitokeza ya ukataji wa miti,serikali katika mkoa wa kilimanjaro kwa nia nzuri kabisa ilisitisha vibali vya ukataji wa miti kwa ajili ya mbao na magogo.
Maamuzi haya hayakuchukuliwa kwa ajili ya manufaa ya mtu binafsi au kwa lengo la kuwakomoa wananchi,bali kuthamini ustawi wa maisha ya jamii yote ya mkoa wa Kilimanjao wakiwemo wakazi wa wilaya ya Hai.
Babu zetu walifanyakazi kubwa ya kupanda miti kwa kasi na ndiyo maana wengi wetu wakati tunazaliwa tulikuta wilaya ya Hai ikiwa na mazingira ya kuvutia yenye mvua za kutosha zilizotusaidia kuendesha shughuli zetu za kilimo na ufugaji kwa ufanisi mkubwa.
Kibaya kilichojitokeza hivi sasa bila ya kuthamini jitihada za wazazi wetu za kupanda miti na kuitunza hivi sasa tumekuwa tukikata miti hii kwa kasi kubwa sana na kuharibu mazingira hali ambayo imesababisha hata msimu wa mvua usiwe wa uhakika huku joto likiongezeka maradufu.
Kutokana na hali hiyo ndipo serikali mkoani Kilimanjaro ikachukuwa maamuzi magumu ya kusitisha vibali vya ukataji wa miti kwa ajili ya mbao na magogo.
Ndugu mwenyekiti,cha kushangaza katika maeneo mengi ya wilaya ya Hai bado kuna baadhi ya vinara wa ukataji wa miti miongoni mwao ni viongozi wenzetu.
Wanaofanya vitendo hivi wanafahamika hivyo ombi
langu la pili kwenu ni kuomba ushirikiano wenu katika kuwafichuwa wanaofanya
hivyo kwa kuwasiliana name moja kwa moja lakini pia kuendelea kutoa elimu
kuhusu umuhimu wa kuendelea kutunza mazingira.
Lakini sanjari na hilo hivi sasa tupo katika kampeni ya upandaji wa miti katika maeneo mbalimbali.
Tumeagiza na kuwaandikia kama wakuu wa shule kuanzisha kitalu ama bustani ya miche ili msimu wa mvua utakapoamza basi tusipate tatizo la miche.
Kama wakuu wa shule hakikisheni mnakwenda kusimamia zoezi la maandalizi ya upandaji wa miti kwa kuwa na vitalu vya miche vya ya kutosha kwa maana mvua zitapoanza kunyesha basi tuanze mara moja zoezi la upandaji wa miti.
1. Utawala bora
Ndugu
Mwenyekiti,Changamoto ya masuala yenye mwelekeo wa utawala bora limekuwa tatizo
kubwa sana katika wilaya yetu kuanzia sisi tulioko ngazi ya wilaya mpaka
viongozi wetu walioko katika ngazi za vijiji.
Aidha Uwajibikaji limekuwa tatizo kubwa sana likitugusa sisi viongozi wa kisiasa mpaka wataalamu wetu wa ngazi mbalimbali huku tatizo kubwa likiwa kusahau majukumu yetu.
Aidha Uwajibikaji limekuwa tatizo kubwa sana likitugusa sisi viongozi wa kisiasa mpaka wataalamu wetu wa ngazi mbalimbali huku tatizo kubwa likiwa kusahau majukumu yetu.
Kwa
upande wa changamoto hii nitaieleza katika maeneo mawili tu ambayo sisi kama wakuu
wa shule na wanajamii katika maeneo yetu tunaweza kusaidia kwa kiasi cha juu
sana.
Changamoto ya kwanza inahusu ufanyikaji wa vikao vya kisheria katika ngazi za vijiji na kata.Hilo limekuwa tatizo kubwa sana katika wilaya yetu.Kila unapita katika vijiji malalamiko makubwa ni ufanyikaji wa mikutano ya vijiji na hasa ajenda inayohusu kusomwa kwa taarifa ya mapato na matumizi.
Kwa uchache sana pia tuna tatizo la ufanyikaji wa mikutano ya kamati za maendeleo za kata yaani WDC katika baadhi ya kata.
Changamoto hizo zote siyo siri zinafahamika vizuri kwa maofisa wetu wa ngazi za tarafa na kata hususani kwa ufanyikaji wa mikutano mikuu ya kijiji na kwa ile ya ngazi ya kata zinafahamika katika halmashauri yetu ya wilaya.
Sasa tunalenga kumaliza tatizo la ufanyikaji wa vikao vya kisheria katika ngazi ya vijiji.Mkiwa wakuu wa shule mnanafasi kubwa ya kushauri na kuelimisha pia kama wasomi hivyo nawaombeni ratiba za vikao vya kisheria katika vijiji vyenu zinafanyika vikiwa na ajenda zote muhimu,mahudhurio na maamuzi.
Lakini kwa upande wa masuala ya utawala bora nimalizie kwa kuwataka nyinyi wakuu wa shule kutojitenga na miradi mbalimbali na badala yake kuhakikisha mnafuatilia kwa ukaribu miradi yote inayotekelezwa katika maeneo yenu iwe ndani ya shule ama katika ngazi ya vijiji.
Naomba nimalize kwa kuwashukuru tena kwa kunipa heshima kubwa ya kunialika katika mkutano wenu huu ambao umenipa fursa kubwa ya kuzungumza nanyi kwa mapana kuhusiana na masuala ya elimu nnchi kwa ujumla pamoja na katika wilaya ya Hai
Changamoto ya kwanza inahusu ufanyikaji wa vikao vya kisheria katika ngazi za vijiji na kata.Hilo limekuwa tatizo kubwa sana katika wilaya yetu.Kila unapita katika vijiji malalamiko makubwa ni ufanyikaji wa mikutano ya vijiji na hasa ajenda inayohusu kusomwa kwa taarifa ya mapato na matumizi.
Kwa uchache sana pia tuna tatizo la ufanyikaji wa mikutano ya kamati za maendeleo za kata yaani WDC katika baadhi ya kata.
Changamoto hizo zote siyo siri zinafahamika vizuri kwa maofisa wetu wa ngazi za tarafa na kata hususani kwa ufanyikaji wa mikutano mikuu ya kijiji na kwa ile ya ngazi ya kata zinafahamika katika halmashauri yetu ya wilaya.
Sasa tunalenga kumaliza tatizo la ufanyikaji wa vikao vya kisheria katika ngazi ya vijiji.Mkiwa wakuu wa shule mnanafasi kubwa ya kushauri na kuelimisha pia kama wasomi hivyo nawaombeni ratiba za vikao vya kisheria katika vijiji vyenu zinafanyika vikiwa na ajenda zote muhimu,mahudhurio na maamuzi.
Lakini kwa upande wa masuala ya utawala bora nimalizie kwa kuwataka nyinyi wakuu wa shule kutojitenga na miradi mbalimbali na badala yake kuhakikisha mnafuatilia kwa ukaribu miradi yote inayotekelezwa katika maeneo yenu iwe ndani ya shule ama katika ngazi ya vijiji.
Naomba nimalize kwa kuwashukuru tena kwa kunipa heshima kubwa ya kunialika katika mkutano wenu huu ambao umenipa fursa kubwa ya kuzungumza nanyi kwa mapana kuhusiana na masuala ya elimu nnchi kwa ujumla pamoja na katika wilaya ya Hai
Nawatakia mafanikio katika mkutano wenu,Mungu
ibariki wilaya ya Hai,Mungu ibariki Tanzania, asanteni kwa kunisikiliza