Mtumishi
katika mnara wa Canton, mrefu kuliko yote nchini China na watatu
duniani kwa urefu, Sarah Xie, akimuonyesha mandhari ya jiji la
Guangzhou, Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, wakati Kinana na
ujumbe wake walipopanda hadi mwisho mnara huo wenye urefu wa zaidi ya
futi 100, Machi 13, 2013. Wengine Kulia ni Katibu wa CCM mkoa wa Mbeya
Maganga Sengelema na Katibu Mkuu wa UVCCM, Martine shigella. Kinana na
ujumbe wake wapo nchini kwa ziara ya siku kumi ya kimafunzo kwa mwaliko
wa Chama Cha Kikomunisti cha China (CPC).
Katibu
Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana na ujumbe wake wakitazama maumbo ya
mandhari ya mji wa Guanzhou, China, yaliyopo ndani ya mnara wa Cnton
wenye urefu wa zaidi ya mita 100, walipotembelea mnara huo, Machi 13,
2013. Kinana na ujumbe wake wapo nchini kwa ziara ya siku kumi ya
kimafunzo kwa mwaliko wa Chama Cha Kikomunisti cha China (CPC).
Katibu
wa NEC, Ushirikiano wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro (kushoto) na
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa mjini Magharibi, Yussuf Mohamed Yusuf wakitaza
bidhaa zinazouzwa kwenye kilele Mnara wa Canton ambao ni mrefu kuliko
yote nchini China ukiwa na urefu wa zaidi ya mita 100, mjini Guangzhou,
China. Dk. Asha-Rose Migiro na Yusuf ni miongoni mwa viongozi
walioambatana na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana katika ziara ya
siku kumi ya kimafunzo kwa mwaliko wa Chama Cha Kikomunisti cha China
(CPC).
Katibu
Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akijaribu uzito wa spika, alipotembelea
Kituo kikubwa cha Sayanasi na Teknolojia cha Ljieafun cha Guangzhou,
kinachojihusisha na ubunifu na utengenezaji 'divaisi' za sauti na
uchanganyaji ragi na matangazo kama ya biashara katika kumbi za muziki
au vituo vya televisheni. Kulia ni Rais wa Kituo hicho, Mike Fung na
wapili kulia ni Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, CCM, Dk.
Asha-Rose Migiro. Kinana na ujumbe wake wapo nchini kwa ziara ya siku
kumi ya kimafunzo kwa mwaliko wa Chama Cha Kikomunisti cha China (CPC).
Katibu
Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akiwa katika mazungumzo na Kamishna wa
maadili na nidhamu wa Chama Cha Kikomunisti cha China (PCP) jimbo la
Dongguan, Cui Jian, kwenye hoteli ya Exibition International mjini
Dongguan, China, Machi 13, 2013. Kinana na ujumbe wake wapo nchini kwa
ziara ya siku kumi ya kimafunzo kwa mwaliko wa Chama Cha Kikomunisti cha
China (CPC).
Katibu
Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akipewa zawadi na Kamishna wa maadili na
nidhamu wa Chama Cha Kikomunisti cha China (PCP) jimbo la Dongguan, Cui
Jian, kwenye hoteli ya Exibition International mjini Dongguan, China,
Machi 13, 2013. Kinana na ujumbe wake wapo nchini kwa ziara ya siku
kumi ya kimafunzo kwa mwaliko wa Chama Cha Kikomunisti cha China (CPC).
Katibu
Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akimpa vipeperushi kuhusu utalii wa
Tanzania, Kamishna wa maadili na nidhamu wa Chama Cha Kikomunisti cha
China (PCP) jimbo la Dongguan, Cui Jian, kwenye hoteli ya Exibition
International mjini Dongguan, China, Machi 13, 2013. Kinana na ujumbe
wake wapo nchini kwa ziara ya siku kumi ya kimafunzo kwa mwaliko wa
Chama Cha Kikomunisti cha China (CPC).
Katibu
Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akizungumza na Maofisa wa Mambo ya Nje
wa Dongguan, China, Sarah Xie (kulia) na Sabina Liu, wakati wa chakula
cha jioni kilichoandaliwa na Kamishna wa maadili na nidhamu wa Chama Cha
Kikomunisti cha China (PCP) jimbo la Dongguan, Cui Jian, kwenye hoteli
ya Exibition International mjini Dongguan, China, Machi 13, 2013.
Kinana na ujumbe wake wapo nchini kwa ziara ya siku kumi ya kimafunzo
kwa mwaliko wa Chama Cha Kikomunisti cha China (CPC).
Katibu
wa NEC, CCM, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro,
akizungumza na Maofiwa wa Mambo ya Nje wa Dongguan Sarah Xie (kulia) na
Sabina Liu, wakati wa chakula cha jioni kilichoandaliwa na Kamishna wa
maadili na nidhamu wa Chama Cha Kikomunisti cha China (PCP) jimbo la
Dongguan, Cui Jian, kwenye hoteli ya Exibition International mjini
Dongguan, China, Machi 13, 2013. Kinana na ujumbe wake wapo nchini kwa
ziara ya siku kumi ya kimafunzo kwa mwaliko wa Chama Cha Kikomunisti cha
China (CPC).
Katibu
Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana na Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa
Kimataifa, Dk. Asha Rose Migiro, wakiwa na viongozi wa Jumuia ya
Watanzania waishio China, alipokutana nao Machi 12, 2013 kwenye hoteli
ya Exhibition Internation mjini Dongguan, China. Kushoto ni, David
Chamala (Katibu) na John Ruhembiza (Mwenyekiti) na kulia ni Abraham
Merishan (Makamu Mwenyekiti) na Abubakar Mwinyi (Katibu Msaidizi).
Kinana na ujumbe wake wapo nchini kwa ziara ya siku kumi ya kimafunzo
kwa mwaliko wa Chama Cha Kikomunisti cha China (CPC).
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia