VATICAN
Makadinali wa kanisa katoliki la
Roma wameanza shughuli ya kumchagua papa mpya. Misa maalum imeandaliwa
katika makao makuu ya kanisa hilo Vatican, St. Peter's Basilica.
Baada
ya misa makadinali wote walio na umri wa zaidi ya miaka 80 wataingia
hekalu ya Sistine ambako upigaji kura utafanyika.
Makadinali hao 115 watafungiwa ndani ya hekalu,
bila mawasiliano na yeyote nje na wataapishwa kuweka siri ya matukio
yote wakati wa uchaguzi huo. Inaaminiwa kuwa shughuli hiyo huenda
ikadumu siku kadhaa.
Mwandishi wa BBC mjini Roma anasema kuwa hakuna
mgombea wa wazi anayetazamiwa kuchukua mahala pa Papa mtakatifu Benedikt
wa kumi na sita. Papa huyo aliwashangaza wengi alipotangaza kujiuzulu
baada ya kuhudumu miaka minane. Yeye ndiye papa wa kwanza kujiuzulu
katika miaka 600 iliyopita.
Maelfu ya waumini wa madhehebu ya katoliki
wamekusanyika nje ya kanisa la St. Peter's Basilica, kufuatilia kwa
karibu shughuli hii muhimu ya kumteua kiongozi mpya wa kanisa.
Makadinali waliochaguliwa watapiga kura mara nne kwa siku hadi pale Papa
mpya atakapo patikana. Kwingineko maelfu ya waumini wanatizama kwenye
televisheni na kusikiliza kwenye redio matukio ya Roma kujua iwapo
wamepata Papa.
Makardinali
wamemchagua Baba Mtakatifu mpya kuliongoza Kanisa Katoliki katika karne
hii ya 21. Vilio vya furaha vilitawala wakati moshi mweupe ulipoonekana
kwenye anga la Vatican City muda mchache uliopita.
Jina halijatangazwa
bado; Papa mpya anatarajiwa kubariki umati uliokusanyika St. Peter's
Square dakika 20-30 zijazo.
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia