Mahmoud
Ahmad Arusha
Jeshi la
polisi mkoani Arusha limafanikwa kukamata madawa ya kulevya aina ya mirungi viroba
51 vyenye uzito wa kilo 352 kwenye matukio mawili tofauti jijini hapa.
Akizungumza
na vyombo mbali mbali vya habari kamanda wa polisi mkoani ha Liberatus Sabas
alisema kuwa tukio la kwanaza limetokea kwenye kata ya Kaloleni majira ya saa 2
Asubuhi kwa vijana wa jeshi hilo kufanikiwa kulikamata gari lenye usajili no
T224 BAQ mali ya George Munge likiwa na viroba 22.
Sabas
alisema kuwa baada ya kupata taarifa kutoka kwa raia wema ndipo vijana wake wa
doria ya pikipiki walipolifuatilia na kufanikiwa kulikamata gari hilo na ndipo
dereva wa gari hilo alipoona anafatiliwa alilitelekeza na kukimbia
kusikojulikana.
Katika tukio
la pili polisi walifanikiwa kukamata viroba 31 vya madawa hayo ya kulevya aina
ya mirungi huko eneo la Enaboishu na kufanikiwa kumakamata mtuhuniwa wa madawa
hayo aliyefahamika kwa jina laBenjamini Babu.
Jeshi hilo
linaendelea na mahojiano na mtumiwa huyo na atafikishwa kwenye mikono ya sheria
baada ya mahojiano hayo huku kamanda wa jeshi hilo mkoani hapa akitoa wito kwa
wafanyabiashara wa madawa hayo kutafuta biashara mbadala ya hiyo.
Sabas
alisema kuwa operesheni ya kuyasaka madawa ya kulevya kwenye mkoa huo ni
endelevu na wala si nguvu ya soda kama wanavyodhani huku akiwapa pongezi
wananchi kwa ushirikiano wanaoutoa kwa jeshi hilo mkoani hapa na hapa nchini
kwa ujumla.
Wakati huo
huo gari lenye namba za usajili T808 ALV limemgonga mwanafunzi na kukimbia
kusikojulikana na likiwa na mwanafunzi huyo ndani hali iliowaacha hoi wakazi walioshuhudia
tukio hilo kwenye makutano ya barabra ya co.Midleton na stand kuu jijini hapa
majira ya saa 6.15 kujua hatma ya mwanafunzi huyo.
Tukio hilo
lililotokea kwenye mataa yaliopo kwenye stand kuu jijini hapa limetoa tahadhari
kwa waenda kwa miguu watumie mataa hayo pindi yanapowaruhusu kuvuka vivuko
hivyo huku wananchi wakitoa lawama kwa madereva mkoani hapa kutoheshimu taa
hizo hali inayoleta matukio kama hayo.
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia