Watu 20 wanashikiliwa na jeshi la polisi mkoani hapa kwa kosa la
kufanya fujo pamoja na kuharibu mali za watu katika tukio la mgomo wa
mabasi ya abiria (dala dala) ulifanyika juzi (Jana) jijini hapa
Akizungumza na waandishi wa habari kamanda wa polisi mkoani hapa
Rebatus Sabas alisema kuwa watu hao wameshikiliwa jana kutokana na
kujihusisha na vurugu mbalimbali pamoja na uharibifu wa mali za watu
ikiwemo kuvunja vioo vya gari aina ya Toyota hiece yenye namba za
usajili T 171 BVE mali ya Edward Clegori (29)msandawe na mkazi wa
mushono.
Alisema kuwa mbali na gari hilo pia jeshi hilo limeshikilia gari moja
aina ya Nissan Caravan yenye namba za usajili T 499 CFV mali ya
Gabriel Thomas Malya ambayo alisema kuwa gari hiyo ilikuwa ilikuwa
inatumika kwa ajili ya kusambaza vijana wahuni ambao walikuwa
wanafanya fujo katika maeneo mbalimbali ya jiji la Arusha pamoja na
kuzuia magari mengine kufanya kazi huku wakiwa wanatoa lugha chafu kwa
abiria pamoja na madereva wengine ambao walikuwa na nia ya kufanya
kazi.
Kamanda Sabas aliwataja baadhi ya watu wanaoshikiliwa na jeshi la
polisi kwa makosa hayo kuwa ni Aizaki Wilfred(23) mchaga ambaye
alisema yeye ni kondakta,Shaibu Khalifani (20)Mchaga ,Gabrieli Thomas
(27)mkazi wa unga ltd,Amani Samosoni mchaga ,said Khalifan Juma (19)
Mpare mkazi wa ngulelo pamoja na Roberty Maico kamugisha (30) muhaya
na nimkazi wa mbauda
Aidha alibainisha kuwa watu hao mpaka sasa wapo mikononi mwa polisi na
pindi upelelezi na ushaidi ukiamilika watafikishwa mahakamani haraka
iwezekanavyo.
matukio haya yametokea baada ya juzi Wakazi wa jiji la Arusha kuonja
joto ya jiwe na adha ya mgomo wa usafiri wa dala dala ukihusishwa na
masuala ya rushwa na kisiasa yanayoendelea kwenye jiji hili huku
wananchi wakitembea umbali wa takribani kilometa 6 kwa miguu kufika
katikati ya jiji hili.
Mgomo huo ulioanza tangia Alfajiri hadi saa tisa mchana uliacha
shughuli za kimaendeleo kusuasua kwa muda huku wakazi wa maeneo
mbalimbali ya jiji la Arusha wakionja joto ya jiwe kutokana na mgomo
huo.
Suala la rushwa kwa askari wa jeshi la polisi kitengo cha usalama
barabarani na suala la kisiasa yamehusishwa moja kwa moja na mgomo huo
ambapo baadhi ya madereva na makondakta waliohojiwa na wanahabari
wamesema kuwa askari wamakuwa wakiwatuma chips kuku kila
wanapowakamata.
Hata hivyo mara baada ya mgomo huo kutokea mkuu wa wilaya ya Arusha
John Mongela alizungumza na waandishi wa habari na kusema kuwa hakuna
aliyejuu ya sheria na kuwa yeyote atakayebainika kuchochea vurugu hizo
zilizoenda sanjari na mgomo hatua kali za kisheria zitafuata mkondo
wake na kuwa hawatafumbia macho wale wote wanaotumia makundi kuwathiri
wananchi kwa manufaa yao ya kutaka umaarufu.
Alisema kuwa wameunda kamati ya muda kutatua masuala yote ya usafiri
wa daladala almaarufu Vifodi jijini hapa na kuwa hawatangoja hadi
mgomo utokee tena kwani kila mwezi watakuwa wakikutana kupeana taarifa
na matukio mbali mbali iliwaweze kuyatatua kwa wakati.

Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia