BENSON MOLLEL ANAZIKWA LEO DARAJA MBILI,JIJINI ARUSHA


Benson Mollel ,enzi za uhai wake.
DSCF8059
Mama mzazi wa marehemu Bi.Suzan Mollel akiwa katika majonzi makubwa
DSCF8054
Baadhi ya Waombolezaji nyumbani kwao marehemu



TUKIO la kufariki kwa aliyekuwa mjumbe wa baraza kuu la Uvccm mkoani Arusha,Benson Mollel(26) limevuta hisia kwa wakazi wengi wa jijini Arusha mara baada ya vifaa mbalimbali kama silaha aina ya bastola,kadi za benki,simu na fedha ambazo kiasi chake hakijajulikana kukutwa katika chumba cha marehemu ndani ya hoteli ya Lush Garden Business iliyopo jijini hapa
Mbali na kujishughulisha na siasa marehemu pia alikuwa akifanya kazi katika kampuni ya madini ya Manga Gems iliyopo jijini Arusha. 
Ndani ya chumba alichofia zilikutwa silaha aina ya bastola,madini ya tanzanite,simu mbili ,kadi za benki na fedha ambazo kiasi chake hakijulikani.
Hata hivyo,utata mzito  umezidi kugubika katika kifo hicho mara baada ya mipira miwili ya kiume(condoms) ambapo mmoja ukiwa umetumika kukutwa katika eneo la tukio.
 Marehemu Mollel alikutwa amefariki majuzi ndani ya hoteli ya Lush Garden Business iliyopo mtaa wa Jacaranda jijini Arusha.

Mashuhuda wamesema kabla ya marehemu kukutwa na mauti alitembelewa na wanawake wawili kwa nyakati tofauti ndani ya chumba chake ambapo mmoja ametambulishwa kwa jina la Nancy na mwingine Mariam.

Kwa upande wake mwenyekiti wa CCM wilaya ya Arusha,Dk Wilfred Ole Soilel alisema kuwa chama chao kimepokea msiba huo kwa masikitiko makubwa kwa kuwa marehemu alikuwa anatumia busara za kuwaunganisha vijana ndani ya chama hicho kwa ukarimu.
DSCF8049
Hoteli alimofia marehemu Benson Mollel
DSCF8044
Gari la Marehemu alilotumia kufika hotelini hapo ambapo kabla ya umauti kumkuta aliegesha gari hilo nyuma ya hotel

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

Previous Post Next Post