MENEJA
wa klabu ya Real Madrid, Jose Mourinho amedai kuwa timu bora ndio
iliyopoteza mchezo baada ya Manchester United ambao walicheza na
wachezaji 10 kutolewa nje katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.
MENEJA wa klabu ya Real Madrid, Jose Mourinho amedai kuwa timu bora ndio
iliyopoteza mchezo baada ya Manchester United ambao walicheza na
wachezaji 10 kutolewa nje katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.
United walitangulia kufunga bao la kuongoza katika mchezo huo wa pili wa
michuano hiyo kabla ya winga wake Nani kutolewa nje kwa kadi nyekundi
na kuipa nafasi Madrid kufunga mabao mawili ya haraka haraka
yaliyofungwa na Luka Modric na Cristiano Ronaldo.Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya mchezo huo ambao Madrid
walishinda kwa mabao 2-1 Mourinho amesema timu yake haikustahili
kushinda mchezo huo lakini soka ndivyo linavyokuwa United
walitangulia kufunga bao la kuongoza katika mchezo huo wa pili wa
michuano hiyo kabla ya winga wake Nani kutolewa nje kwa kadi nyekundi na
kuipa nafasi Madrid kufunga mabao mawili ya haraka haraka yaliyofungwa
na Luka Modric na Cristiano Ronaldo. Akizungumza na waandishi wa habari
mara baada ya mchezo huo ambao Madrid walishinda kwa mabao 2-1 Mourinho
amesema timu yake haikustahili kushinda mchezo huo lakini soka ndivyo
linavyokuwa wakati mwingine.
Mourinho alikisifu kikosi cha United kinachonolewa na Sir Alex Ferguson
akidai kuwa kilijipanga na kucheza vyema katika mchezo huo na kama
isingekuwa kadi nyekundu aliyopewa hadhani kama wangepata ushindi huo.
Nani (katikati) baada ya Refa Cuneyt Cakir kumpa kadi nyekundu..
Rio Ferdinand akionana uso kwa uso na Refa baada ya mechi kuisha jana usiku old trafford.
Patrice Evra (Kulia) na Ashley Young (katikati)wakiondoka uwanjani kwa jaziba kubwa baada ya refa kuwaangusha kwa kadi nyekundu aliyompa Nani.