Tukio la
kusimamishwa kwa mwenyekiti wa wa
jumuiya ya umoja wa vijana wa Chama Cha Mapinduzi(Uvccm) wilaya ya Arumeru
mkoani Arusha,Boniphace Mungaya limehusishwa na mlengo wa siasa za makundi
ndani ya chama hicho tawala.
Mungaya,alisimamishwa
ili kupisha uchunguzi mnamo oktoba mwaka jana baada ya kuandikiwa barua na
katibu wa CCM mkoani hapa,Mary Chatanda akituhumiwa kuwa ni mlinzi wa
mwenyekiti wa Chadema taifa,Freemam Mbowe na mara kwa mara amekuwa akionekana
naye.
Taarifa
kutoka vyanzo mbalimbali vya habari vimedai kwamba Mungaya anahusishwa na
mtandao wa mbunge wa Monduli,Edward Lowasa ambaye anatajwa kuwa ni miongoni mwa
wanachama wa CCM wanaowania mbio za urais mwaka 2015.
Vyanzo hivyo
vya habari vimemtaja Chatanda ambaye alimwandikia barua ya kumsimamisha Mungaya
kuwa anahusika katika kundi la waziri ya mambo ya nje ya ushirikiano wa
kimataifa,Bernad Membe ambaye naye anatajwa kuwa miongoni mwa vigogo
wanaopigana vikumbo kuwania urais mwaka 2015.
Hatahivyo,taarifa
mbalimbali zimeeleza kuwa kusimamishwa kwa mwenyekiti huyo kulitokana na
kuangushwa vibaya kwa aliyekuwa mgombea wa Uvccm wilayani Arumeru ,Lightness
Msemo ambaye ametwaja kuungwa mkono na mtandao wa Membe akiwemo Chatanda.
Wachambuzi
wa masuala ya kisiasa mkoani Arusha
wamesema kwamba siasa za makundi ndani ya chama hicho ndiyo sababu kuu
iliyopelekea kusimamishwa kwa Mungaya ambaye kwa sasa anasubiria uamuzi wa
halmashauri kuu ya CCM mkoani Arusha ambayo inatajwa kukaa hivi karibuni
kumaliza mzizi wa fitina.
“Ngoja
tukwambie Mungaya ameponzwa na siasa za makundi ndani ya chama chetu yeye yuko
mtandao wa Lowasa na Chatanda alikuwa na chaguo lake ambaye ni Msemo lakini
baada ya kuangushwa kwenye uchaguzi wakaamua kumuundia fitina akasimamishwa”walisema
baadhi ya makada wa CCM wilayani Arumeru
Hatahivyo,Mungaya
alipotafutwa na gazeti hili ili aweze kujibu madai hayo alikataa kuzungumzia
chochote huku akisema kuwa kwa sasa anasubiri uamuzi wa halmashauri kuu ya CCM
mkoani Arusha ili aweze kujua hatma yake.
Naye,Chatanda
alipotafutwa hivi karibuni na gazeti hili alisema kuwa suala hilo liko ndani ya
chama na haliwezi kujadiliwa kwenyen vyombo vya habari.
Mwenyekiti
wa CCM mkoani Arusha,Onesmo Ole Nangole alipoulizwa alisema kwamba kwa sasa
yuko mapumzikoni wilayani Longido kwa matibabu na kuomba aachwe kwanza mpaka
pale atakapopata nafuu.
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia