Kocha wa Taifa Stars mara baada ya kumaliza mbio za Kilimanjaro Marathon
katika uwanja wa Ushirika (Moshi) akiwa amepanga mstari wa wanariadha
waliokuwa wakimaliza mbio.
Nimevutiwa na washiriki wengi walioshiriki ambao sio mabingwa wa liadha bali wamepima uwezo wao wa kiafya.
Nimevutiwa na washiriki wengi walioshiriki ambao sio mabingwa wa liadha bali wamepima uwezo wao wa kiafya.
Victor Machota nikifuatilia kwa karibu mambo yote yaliyokuwa yakiendelea katika Kilimanjaro Marathon 2013, mengi niliyaona, nilizungumza na baadhi ya washindi wa mbio hizo kutoka Tanzania na Kenya pia.
Natumai utapenda kujua nini walichokisema washindi hao, pia Ommy Dimpoz na TMK Wanaume + Bi Cheka... fuatilia blog www.victormachota.blogspot.com hii utasikia sauti zao mmoja mmoja mwanzo mwisho.
Natumai utapenda kujua nini walichokisema washindi hao, pia Ommy Dimpoz na TMK Wanaume + Bi Cheka... fuatilia blog www.victormachota.blogspot.com hii utasikia sauti zao mmoja mmoja mwanzo mwisho.
Washiriki wa Kimanjaro Marathon 2013 wakiwa kwenye mstari mara baada ya
kumaliza mbio hizo ambazo kwa wanariadha wengine walikuwa bado
wanawasili.
Jamaa huyu huenda ukafikiri ni mpita njia tu, lakini sio hivyo huyu ni
mmojawapo wa washiriki wa riadha ya Kilimanjaro Marathon 2013.
Nilivutiwa na washiriki wengi ambao sikutegemea kama nao wangeshiriki,
ni wito kwa kila mwenye uwezo kushiriki mashindano haya..... oooh!! I
did'nt know about it!!!!!
Wageni pia walipata nafasi ya kushiriki na watanzania wengi katika mbio hizi za Kilimanjaro Marathon.
MWANARIADHA wa
Kitanzania, Sarah Ramadhani, jana aliibuka shujaa katika mashindano ya mwaka
huu ya mbio ndefu za Kilimanjaro Premium Lager Marathon, baada ya kuibuka
mshindi katika mashindano ya kilomita 21, (nusu marathon), kwa upande wa
wanawake katika mbio zilizofanyika mjini Moshi, mkoani Kilimanjaro.
Sarah alishinda mbio
hizo baada ya kukimbia kwa dakika 1:13:05 na kujipatia medali ya dhahabu baada
ya kuwabwaga wenzake wakiwemo Wakenya ambao wamekuwa wakitawala mbio hizo
katika miaka ya hivi karibuni.
Katika mbio hizo
ambazo mwaka huu zimeweka rekodi ya kuwa na washiriki zaidi ya 6,800, Vicoty
Chepkemoi, kutoka Kenya alishika nafasi ya pili baada ya kukimbia kwa dakika
1:14:34, ambapo Mtanzania mwingine Failuna Matanga, alishika nafasi ya tatu kwa
kukimbia kwa dakika 1:15:35.
Hata hivyo wakenya waliendeleza ubabe wao, baada ya
wanariadha wake kushika nafasi ya kwanza katika mbio za kilomita 42 na kilomita
21 wanaume, pamoja na nafasi ya kwanza katika kilomita 42 upande wa wanawake.
Katika mbio za kilomita 42 wanaume, Kipsang Kipkemoi
alishika nafasi ya kwanza kwa kukimbia dakika 2:14:56 na kufuatiwa na mkenya
mwenzake Julius Kilimo, aliekimbia kwa dakika kwa dakika 2:15:44 ambapo mkenya
mwingine Dominic Kiangor alishika nafasi ya tatu kwa kukimbia dakika 2:16:25.
Kwa upande wa wanawake, mkenya Edna Joseph, alishinda mbio
hizo pale alipomaliza kwa dakika 2:39:05 na kufuatiwa na Eunice Muchiri,
(Kenya), aliekimbia kwa dakika 2:41:00 na watatu alikuwa ni Fridar Too,
aliekimbia kwa dakika 2:44:04.
Akiongea muda mfupi baada ya kuwazawadia washindi, Waziri wa
Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk. Fenela Mukangara, aliahidi
ushirikiano wa serikali katika kuendeleza michezo hapa nchini.
“Nichukue nafasi hii
kuwapongeza wadhamini wa mbio hizi, Kilimanjaro Premium Lager pamoja na
wadhamini shirikishi mbalimbali wa mashindano haya wakiongozwa na mdhamini
mkuu, kwani mbali na kuibua na kukuza vipaji vipya, mashindano haya yametokea
kuwa mchango mkubwa katika kuitangaza Tanzania na kukuza uchumi wa Kilimanjaro
na nchi kwa ujumla kutokana na kushirikisha watu wengi kutoka ndani na nje ya
nchi”, alisema.
Aliwataja wadhamini wengine kuwa ni pamoja na Vodacom
Tanzania, GAPCO, Tanga Cement, CFAO Motors, KK Security, Keys Hotel, TPC Sugar,
Tanzanite One, New Arusha Hotel, UNFPA, Fastjet na Kilimanjaro Water.
Aidha alitoa changamoto kubwa kwa viongozi wa riadha nchini
kuhakikisha wanariadha wa Tanzania wanaandaliwa vyema na mapema ili kuendeleza
ushindi, ambapo alisema ushindi wa Sarah na Failuna Makanga na mfano mzuri wa
matayarisho mema.
Kwa upande wake Meneja wa
Bia ya Kilimanjaro Premium Lager, George Kavishe alisema kuwa mbio hizi
zimeweza kuleta hamasa kwa watu mbalimbali kushiriki mchezo wa riadha kwani Kilimanjaro
Marathon ni tukio pekee la kimichezo ambalo linatoa fursa kwa watu wote
kushiriki. “Tutaendelea kuwekeza katika riadha kwa kadri tuwezavyo kwa sababu
Kilimanjaro Marathon sio tu kwa sababu imeishakuwa tukio linalosubiriwa na
wanariadha wetu kila mwaka lakini pia ni tukio ambalo limeendelea kuitangaza
nchi yetu kimataifa”, alisema.
Kavishe alisema tangu mbio hizi zilipofanyika kwa mara ya
kwanza mwaka 2003, Kilimanjaro Premium Lager iliamua kudhamini tukio hili kwa
kuzingatia umuhimu wake kwa nchi yetu katika kukuza na kuendeleza mchezo wa
riadha na vilevile kuutangaza Mlima Kilimanjaro ambao ni fahari ya Watanzania
kama ilivyo bia yao ya Kilimanjaro Premium Lager.