Waziri mkuu aliyejiuzulu Edward Lowassa
amefanikisha kukusanywa kwa Sh85 milioni katika harambee ya kukusanya
fedha kwa ajili ya kutatua tatizo la ajira kwa vijana, mkoani Arusha.
Harambee hiyo iliyofanyika juzi, iliandaliwa na Umoja wa Waendesha Pikipiki (Uwapa) wa Jiji la Arusha.
Akizungumza katika harambee hiyo, Lowasa ambaye
pia ni Mbunge wa Monduli, aliwataka vijana kujiepusha na ushawishi wa
wanasiasa wanaowarubuni ili kushiriki katika maandamano yasiyokuwa na
tija.
Badala yake, aliwataka wajikite katika kuzungumzia
maendeleo yao. Alisema fedha zilizopatikana katika tukio hilo, ni vyema
zikatumika katika kukopeshana ili kupanua mitaji ya biashara zao.
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia