Ofisa wa polisi jamii Tarafa ya Moipo Mkoani
Manyara,Amiri Mlemba akikabidhi mpira kwa mabingwa wa soka wa Wilaya ya
Simanjiro,timu ya Middle Age ya Mji mdogo wa Mirerani kwenye uwanja wa Barafu
TIMU ya Middle Age ya Mji mdogo wa Mirerani
ambao ni mabingwa wa soka wa Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara,wamepatiwa
mpira na Ofisa Polisi Jamii wa Tarafa ya Moipo ili wajiandae vizuri na ligi ya
mkoa huo.
Akikabidhi mpira huo jana kwenye uwanja wa
Barafu wa Mji mdogo wa Mirerani,Ofisa wa Polisi jamii Tarafa ya Moipo,Amiri
Mlemba alisema lengo lao ni kuunganisha vijana na dhana ya ulinzi shirikishi na
polisi jamii.
Mlemba alisema kupitia vijana hao
kujishughulisha na michezo hivi sasa watajiweka kwenye nafasi nzuri ya kujiunga
na ajira isiyo rasmi kuliko kuwa kwenye magenge ya wahuni na wavuta bangi.
Alisema kupitia ofisi yake wanajipanga kutoa
sare za michezo kwa timu hiyo ambayo ni mabingwa wa wilaya ya Simanjiro na
inajiandaa kushiriki ligi ya mkoa wa Manyara inayotarajia kuanza hivi karibuni.
Naye,kocha wa timu hiyo Ally Ajemi alitoa
shukrani kwa Ofisa wa polisi jamii wa kwa kuwapa mpira huo utakaowasaidia
kujiweka vizuri kwa mazoezi kwa wakati huu wanaposhiriki ligi ya kombe la
Diwani Lucas Zacharia.
“Tunashukuru kwa msaada huu wa mpira kwani
umekuja kwa wakati muafaka ukizingatia hivi sasa tunashiriki kwenye ligi ya
Kombe la Diwani na pia tunajiandaa kushiriki ligi ya mkoa wa Manyara,” alisema Ajemi.
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia