BREAKING NEWS

Wednesday, March 13, 2013

VATICAN YAANZA MCHAKATO WA KUTEUWA PAPA MPYA SIKU YA KWANZA NDO HIYO IMETOKA HOLA TUCHEKI LEO I

Enela kibaraza katika kanisa la Mt. Petro ambapo Papa mpya ataonekana kwa mara ya kwanza.
Enela kibaraza katika kanisa la Mt. Petro ambapo Papa mpya ataonekana kwa mara ya kwanza. 
 

Makardinali 115 wa Kanisa Katoliki wanaanza kumchagua Baba Mtakatifu Vatican

Moshi mweusi unaoonekana juu ya paa la nyumba ambayo makardinali wanakutana. Moshi huo unamaanisha bado Papa hajapatikana. Kukutana tena kesho mpaka moshi mweupe utakapotokea kutoka kwa jina lolote.
Siku ya kwanza ya kumchagua Papa imetoka patupu mara baada ya moshi mweusi kutanda kwenye paa la nyumba waliyokutana makardinali katika kumchagua kiongozi wao mkuu mpya. Kwa maana hiyo makardinali hao watakutana tena jumatano baada ya ibada ili kufaya uchaguzi, wakitumainia moshi mweupe kutoka kwa jina mojawapo la watakaopigiwa kura.

Eneo ambalo makardinali wanakutana kumchagua Papa mpya.
Makardinali wakijiandaa na shuhguli yao
Waamini wakifuatilia shughuli ya kumchagua Papa mpya kwenye skrini ya ukutani Vatican, St Peters Square.
Kardinali Mnigeria, Peter Kodwo Appiah Turkson, akiwa kwenye ibada ya kuombea uchaguzi wa Papa.

Makardinali wakiwa kwenye ibada ya kuombea kumchagua Papa mpya
Nguo tatu za urefu tofauti, na maboksi ya viatu yakiwa tayari, kumsubiri Papa mpya. 
Macho na masikio ya wakatoliki yanaelekea Vatikan  ambapo makardinali 115 wanaanza kumchagua Papa mpya Jumanne.

Mkutano wa makardinali utafanyika kwa faragha katika kanisa la Sistine na hautamalizika mpaka Papa mpya atakapopatikana . Hakuna anayesema ni muda gani utachukua . Lakini dunia itajua wakati kanisa litakapokuwa na kiongozi mpya wakati moshi mweupe utakapotoka kwenye  sehemu maalum ya kutoa moshi uliowekwa kwenye dari ya kanisa hilo.


Atakayechaguliwa lazima apate kura 77 theluthi mbili ya walio wengi. Hakuna anayeongoza  moja kwa moja  katika nafasi hiyo kwa sasa.


Wakati kanisa katoliki linachagua Papa mpya , linafuata utaratibu ambao umekuwepo bila ya  kubadilika kwa karne nyingi. Tofauti pekee safari hii ni kwamba Papa aliyepita Benedict XVI bado yuko hai.


Katika jioni ya kwanza kura ya kwanza  itapigwa baada ya hapo watapiga kura nne kila siku,   mbili asubuhi na mbili jioni. Mgombea atakayefanikiwa anahitaji theluthi mbili ya kura zilizopigwa.

Share this:

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

 
Back To Top
Copyright © 2014 MOUNT KILI NEWS. Designed by OddThemes | Distributed By Gooyaabi Templates