Polisi wakionesha silaha na vifaa vilivyokamatwa kutoka kwenye nyumba
ya maficho ya al-Shabaab mjini Mogadishu siku ya Jumatatu (tarehe 4
Machi). [Abdi Said/Sabahi]
Vikosi vya usalama vya Somalia vimewakamata watu 13 wanaoshukiwa kuwa
wanachama wa al-Shabaab katika operesheni ya usalama kwenye wilaya ya
Yaqshid mjini Mogadishu siku ya Jumatatu (tarehe 4 Machi).
Washukiwa hao walikamatwa wakati wa safishasafisha ya usalama kwenye
wilaya hiyo iliyowapelekea maafisa wa usalama kwenye nyumba ya maficho
katika viunga vya Towfiq, alisema kamanda wa Usalama wa Taifa wa
Benadir, Kanali Khalif Ahmed Ereg. Polisi pia walikamata mikanda ya
mabomu, mabomu ya kurushwa kwa mkono, ving'amuzi vya simu za mkononi,
kompyuta za mkononi na vifaa vingine kwenye nyumba hiyo.
Zaidi ya watu 100 walikamatwa kwenye operesheni hiyo ya usalama ya
siku ya Jumatatu, lakini wote hawakukutwa na makosa na waliachiwa baada
ya kufanyiwa mahojiano, alisema Ereg.