Kibarua cha kocha wa Reading, Brian McDermott kimeota majani, katika mazingira yanayoonesha kwamba amelazimishwa kujiuzulu.
McDermott
(51) ndiye aliyewaongoza Reading kupanda daraja msimu uliopita,
akachaguliwa kuwa kocha bora wa mwezi hivi karibuni, lakini tangu hapo
timu yake imepoteza mechi nne mfululizo.
“Mmiliki Owner Anton
Zingarevich anamshukuru Brian kwa kazi yake. Utafutaji wa kocha mpya
unaanza mara moja, na matarajio ni kujaza nafasi hiyo haraka
iwezekanavyo.
“Brian
aliiwezesha klabu kupanda Ligi Kuu mwaka jana, ikiwa ni mara ya pili tu
katika historia ya klabu…hata hivyo, kutokana na hali ilivyo, mmiliki
Zingarevich ameona ulazima wa kufanya mabadiliko,” taarifa ya klabu inasema.
McDermott alijiunga Reading 2000 akifanya kazi chini ya Alan Pardew ambaye sasa ni kocha wa Newcastle United.
Mwaka
2009 baada Reading kumfukuza kazi kocha wao, Brendan Rodgers (sasa bosi
wa Liverpool wanaofanya vizuri), McDermott alipewa ukocha wa muda kabla
ya kuwa kocha kamili.
Reading
wanashika nafasi ya 19 kati ya 20 zinazoshiriki Ligi Kuu, wakiwa na
pointi 23 sawa na Queen Park Rangers (QPR) wanaoshika mkia na
wamebakisha mechi tisa kumaliza ligi.
*************************************
UNITED WAMTEGA CR7...
Manchester United
wanatarajia kuongeza shinikizo ili kumpata tena mchezaji wao wa zamani,
Cristiano Ronaldo kutoka Real Madrid. Inasemekana kilifanyika kikao
kizito mwishoni mwa wiki kati ya maofisa wa Man U na Nike, kampuni
inayomdhamini Ronaldo kwa viatu na mambo mengine.
Nike hawapendezwi kuona Ronaldo akitangaza bidhaa za kampuni shindani
kama Adidas na nyinginezo klabuni Real Madrid, hivyo wanataka kuona
akijiunga na klabu kubwa inayovaa nembo zao. Fitna inayogharimu pauni
milioni 75 inaelezwa ilitengenezwa ili kumng’oa mpachika mabao huyo
mahiri wa Bernabeu, lakini hakuna uhakika...