Mkurugenzi wa kampuni ya MAG Promotion entertainment east africa ili Maganya Fadhakiongea na waandishi wa habari kuhusiana na wazo lake la kuanzisha mara all star
KAMPUNI ya Mag Promotions na Entertainment East Africa
inakusudia kuwaunganisha wasanii wote wa muziki wa Injili na wale wa kizazi
kipya wanaotokea mkoani Mara ikiwa ni juhudi za kuiga mfano wa wasanii wanaunda kundi la Kigoma All
Stars.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na mkurugenzi wa kampuni
hiyo,Maganya Fadhili alisema kuwa kuwa kampuni yake inajishughulisha na masuala ya
kuwapromoti wasanii mbalimbali nchini ameona ni bora awaunganishe wasanii wanaotoka mkoani
Mara kwa kuzingatia na yeye ni mzaliwa wa mkoani humo.
Fadhili,ambaye alivunja rekodi ya kumleta msanii Jose
Chamilione mwaka 2002 na kumtembeza mikoa 17 hapa nchini alisema kwamba huu ni
wakati wa wasanii kutoka mkoani Mara kama Judith Wambura”Lady Jay Dee” kuungana
kwa pamoja ili kujiletea maendeleo.
Hatahivyo,alisema tayari alishafanya utaratibu wa
kuwasiliana na baadhi ya wasanii
wanaotoka mkoani ambapo wamemsapoti na kusisitiza kuwa pindi utaratibu ukishakamilika
watakubalina kufanya kazi kwa ushirikiano.
Alitoa wito kwa mapromota wa kazi za wasanii wanaotoka
mkoani Mara kama Jospeh Kusaga na Chief Kiumbe kumsapoti katika harakati hizo
ili kuutangaza mkoa wa Mara aliodai una fursa nyingi za kiuchumi.
“Natoa wito kwa mapromota mbalimbali wa kazi za muziki kama Kusaga
na Chief Kiumbe wanaotoka mkoani Mara tuunganishe nguvu kwa pamoja ili
kuutangaza mkoa wa Mara”alisema Fadhili
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia