KAMPUNI YA MEGATRADE YATOA MSAADA WA SUFURIA ZA KUPIKA KATIKA SHULE ZA KATA YA UNGA LTD

Picha ikionyesha wafanyakazi wa kampuni ya Megatratide Investmet Limited wakiwa na diwani wakata ya Ungaltd wa kwanza kushoto ni Administration officer wa kampuni hiyo akifuatiwa na diwani wa kata ya Unga ltd Issa Saidi wa tatu ni Afisa elimu wa katia ya Unga ltd Ester Londriki wa kwanza kulia ni Kakwaya Ruji  Operation officer  wa  kampuni hiyo akifuatiwa na Joilos Joseph sales and marketing activation

picha juu na chini makabidhiano ya sufuria

picha sales and marketing activation Joilos Josephy wa kwanza kulia na diwani wa kata ya Ungaltd wakipeana mikono mara baada ya makabidhiano
KAMPUNI YA megatrade investment limited  imetoa msaada wa sufuria za kupikia zenyethamani ya zaidi ya shilingi milioni kwa shule mbili zilizopo ungaltd ilipo ndani ya jiji la Arusha.

Akikabidhi msaada huo meneja masoko na mauzo wa kampuni hiyo Jailos Joseph alisema kuwa kampuni hiyo imeamua kutoa msaada huo kutokana na ombi ambalo walipelekewa na diwani wa kata hiyo  .

Alibainisha kuwa walipelekewa ombi la kutoa msaada wa chakula kwa shule hizo mbili kwani wanafunzi wamekuwa wanashinda njaa hali inayowapelekea hata kutofanya  vizuri katika masomo yao huku wengine wakiwa wanaanguka anguka katika saa za vipindi kutokana na njaa hivyo mara baada ya kusikiwa matatizo hayo ya wanafunzi wao kama kampuni ya megatrade waliamua kutoa msaada huo .

"kweli sisi tumekuwa tukitoa ushirikianao katika mambo mengi ya kijamii lakini mara tu baada ya kusikia kuwa watoto wa shule za ungalimetedi wamekuwa wanapata shida ya kuanguka darasani wengine wanakuwa watoro wa kuja shule huku wengine wakiwa wanashindwa kusoma kwa ajili ya njaa tukaamua kukaa na kuamua kuja kutoa msaada huu na hapa sio mwisho tutaendelea kuwasaidia siku hadi siku ili kuweza kuwawezesha vijana wetu kupata elimu ya kutosha"alisema Joseph

Msaada huo umekuja baada ya uongozi wa kata pamoja shule kuandika barua kwa kampuni hiyo kuomba msaada wa sufuria mbili za ujazo wa lita 100 na lita 200 kwaajili ya kuwapikia chakula  wanafunzi wakiwa shuleni,  kutokana na wanafunzi kushinda njaa kwa muda mrefu na kushindwa kumudu masomo yao vizuri hali inayopelekea  wakati mwingine kuanguka na kupoteza fahamu na wengine kutoroka shule kutokana na njaa
Akipokea msaada huo diwani wa kata ya Ungaltd Issa Saidi alisema kuwa wanashukuru kampuni hiyo kwa kuwapa msaada huo kwani watakuwa wamewapunguzia tatizo kubwa ambalo lilikuwa linawakabili kwa kipindi cha mda mrefu huku akisema kuwa anaimani kabisa tatizo la watoto kuanguka mashuleni pamoja na kutoroka na kutouzuria shule litaisha kwakuwa watotowatakuwa wamepata mlo wa mchana

Alisema kuwa katika kaipindi cha nyuma utoro ulikuwa unaongezeka siku hadi siku lakini kwa sasa wanaimani kabisa kuwa utoro utapungua katika shule hizi mbili zilizopo katika kata hii na
hali ya awali ambayo ilikuwa inaonekana kuwa mbaya itapungua na hii itasaidia kuendeleza kizazi hiki kwa kuwapa watoto elimu bora .
"napenda pia kuwaambia kamati ya maendeleo ya kata pia inawashukuru sana wameona mmeguswa na kuona watoto hawa wanaitaji kitu kutoka kwa wadau wa kata hii na wanashukuru sana kwa vifaa hivi na napenda kuwaambia kuwa waendelee kujitokeza kusaidia katika tatizo lolote lilile linalotokea katika kata hii na sio nyie tu bali hata wadau wengine waliopo katika kata hii tunawaomba waelele kusaidia katika shughuli za maendeleo.
Aidha  alisema kuwa kwa sasa  wanafanya utaratibu wa mkutano wa kamati ya shule , kata, wazazi na wanafunzi wote kuwaonyesha na kuwakabidhi msaada huu ambapo watawaita  na kuwatambulisha kwa wazazi ili wawajue wadau ambao wanawasaidia katika kata yao  na kuwaambia  kuwa wao ndo waliotoa  msaada huo huku .

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

Previous Post Next Post