BARA LA AFRIKA LATAKIWA KUJIPANANGA KUANDAA MIKAKATI YA KIUCHUMI
Bara la
Afrika limetakiwa kujipanga katika kuandaa mikakati ya kiuchumi na kuangalia mdororo wa kiuchumi
unaoukumba ulimwengu kwa sasa likiwemo bara la ulaya kama changamoto ya
kupambana na umaskini katika bara letu ilikufikia mafanikio waliofikia nchi
kama China na Brazili.
Hayo
yalisemwa na raisi wa jamhuri ya muungano wa Tanzania dkt.Jakaya Kikwete wakati
akifungua mkutano wa mwaka wa benki ya maendeleo ya Afrika(AfDB) jijini Arusha
na kuwataka benki hiyo ya maendeleo kuwa mstari wa mbele kulikomboa bara hili
kiuchumi.
Dkt.Kikwete
alisema kumekuwa na miundombinu mibovu,kilimo kisichokidhi soko la ndani
sanjari na kutotumia rasilimali zetu vizuri huku kunaliangusha bara hili
kutopiga hatua za kiuchumi na kulifanya kuwa tegemezi kwa wahisani ndani ya
bajeti zao.
Akawataka
washiriki wanaoshiriki mkutano huo kutoa majawabu ya hali za kiuchumi
yanaolikumba bara hili kwa sasa ilikufikia katika kilele cha mafanikio ya
kiuchumi waliyonayo nchi zilizoendelea pia akatoa shukurani kwa wahisani
wanaoendelea kuzisaidia nchi zetu.
Nae raisi wa
benki ya maendeleo ya afrika Donarld Kaberuka alisema kuwa matumizi mabaya ya
madaraka sambamba na vita vya wenyewe kwa wenyewe yanalifanya bara hili kuwa
nyuma kimaendeleo na kuwataka kuwa na soko la pamoja la kimataifa kwa watafuta
bidhaa na malighafi.
Kaberuka alisema
kuwa kuwepo na mfumo wa kibiashara za kienyeji kati yetu nchi kwa nchi na
baadae kuelekea katika masoko ya kimataifa kutafanya kuwa na mfumo sahihi
wakuweza kujua hali la soko letu na jinsi ya kupanga bei.
“Naona
fahari kusafiria bara bara kutoka Kenya hadi hapa Tanzania ambayo sisi kama
benki tumeichangia uwepo wake kwa
kufanikisha barabara ya Nairobi hadi Arusha.
Mkutano huo
wa siku tano unafikia kilele chake kwa uzinduzi wake ulifanywa na raisi Kikwete
na mgeni wake raisi wa Aivory Coast Alasane watara na magavana kutoka mataifa
wanachama wa benki hiyo na wageni mbali mbali mashuhuri kutoka mataifa mbali
mbali ulimwenguni.
0 Comments:
إرسال تعليق
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia