PREMIER PALACE YAFUNGULIWA RASMI ARUSHA
![]() |
MKURUGENZI WA HOTEL, ALEX MARIWA AKIONGEA WAKATI WA UZINDUZI
WAFANYABIASHARA jijini Arusha wametakiwa kuacha mashindano na badala
yake washirikiane katika kuhakikisha wanaongeza ajira na kukuza uchumi.
Hayo yalisemwa juzi na mkurugenzi wa hoteli ya kitalii ya Premier
Palace, Alex Mariwa alipokuwa akizungumza katika hafla fupi ya uzinduzi
wa hoteli hiyo iliyopo Makao Mapya kata ya levelosi.
Alisema kuwa watajitahidi kuhakikisha kuwa mahitaji ya vitu mbalimbali
vinavyohitajika kwenye hoteli hiyo vinanunuliwa Arusha na vitongoji
vyake ili kuweza kuongeza kipato cha wananchi na kujenga mahusiano mema.
“Tupo hapa Arusha si kwa mashindano ila kufanya kazi pamoja na wenzetu
wenye mahoteli na Tour Operators (mawakala wa utalii) kwa manufaa yetu
wote kwa nia ya kuongeza soko la ajira na kukuza uchumi wa Taifa letu”
alisema Mariwa.


0 Comments:
إرسال تعليق
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia