Rais Donald Kaberuka
BAJETI nyingi za Nchi za Afrika zimekuwa tegemezi kwa kutegemea wahisani na Nchi kutozikidhi bajeti hizo jambo
ambalo linapelekea kutumia rasilimali za Nchi vibaya kwa maslahi ya wahisani
Pia SERIKALI
imetakiwa kutumia Utawala bora wa fedha kwa wananchi wake na matumizi sahihi ya
mali Asili kwa manufaa ya vizazi vijavyo na kuitumia demokrasia katika kukuza
pato la wananchi wake hapa Nchini
Hayo
yamesemwa na Waziri wa Elimu mafunzo ya Amali kutoka (SMZ)Ally Juma
Shamuhuna wakati akizungumza na vyombo vya habari jana jijini Arusha kwenye
mkutano wa Benki ya Maendeleo ya Afrika(AfDB)
Alisema kuwa
wamekuja kujifunza na leo wamejifunza juu ya suala zima la Demokrasia
inavyoweza kukuza uchumi wa Nchi yeyote Sanjari na utawala bora wa matumizi ya fedha za serikali
na kuwa wanaelekea kwenye bajeti ya mwaka wa fedha 2012-13 ambapo watakuwa
wamepata uzoefu
Waziri huyo
alisema kuwa serikali yeyote itakayo fuata mambo matatu na kuyajali kwa maslahi
ya wananchi wake huku akitaja kuwa Utawala bora wa fedha,Matumizi sahihi ya
Demokrasia sanjari na Matumizi ya Mali Asili zitaifanya serikali hizo kutokuwa
tegemezi kwa wahisani
“Mashirika
haya ya fedha ulimwenguni hayatoi fedha bure lazima watangulize maslahi yao
hali inayopelekea Nchi zilizofadhiliwa kubaka demokrasia na wananchi wake
kuendelea kuwa maskini”alisema Bw.Shamuhuna

0 Comments:
إرسال تعليق
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia