WATAALAMU WA MAWASILIANO NA UCHUKUZI WATAKIWA KUTAFUTA UMBUZI WA TATIZO LA UDUNI WA MIUNDO MBINU


WAZIRI wa Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe amewata wataalamu wa fedha,
mawasiliano na uchukuzi kutafuta ufumbuzi wa tatizo la uduni wa
miundombinu unaodidimiza uchumi barani Afrika.

Aliyasema hayo wakati akifungua mkutano wa mwaka wa Taasisi za fedha zinazofadhili maendeleo
barani Afrika (AADFI), unaoenda sambamba na mkutano wa Magavana wa
Benki ya Maendeleo Afrika unaofanyika Jijini Arusha , Dk Mwakyembe
alisema mipango ya maendeleo na kukuza uchumi haiwezi kufanikiwa iwapo
miundombinu haitaboreshwa kurahisisha usafirishaji.

Alisema hadi sasa nchi nyingi barani Afrika zinatumia barabara kama
njia kuu ya usafirishaji badala ya reli ambayo licha ya kuwa na
gharama nafuu lakini pia husafirisha kiwango kikubwa cha mizigo
kulinganisha na barabara na kuwataka wataalamu hao kutafuta njia ya
kupata fedha za ndani kugharamia ujenzi na ukarabati wa miundombinu.


“Kukosekana na kutofanyia matengenezo ya mara kwa mara barabara zetu
kunakwaza mawasiliano na hivyo kupunguza kasi ya kujiletea maendeleo
kutokana na ukweli kwamba mawasiliano ndiyo nyenzo muhimu kiuchumi,”
alisema Dk Mwakyembe

Alisema uduni wa njia za mawasiliano huchangia gharama kubwa ya
usafirishaji ambayo humwangukia mtumiaji wa mwisho ambaye ni mwananchi
wa kawaida anayelazimika kununua bidhaa kwa bei ya juu kulinganisha na
wanaoishi kwenye nchi zilizoendelea kimiundombinu.

Dk Mwakyembe alisema tatizo la miundombinu ni moja ya changamoto kwa
serikali zote za Afrika katika juhudi za kukuza uchumi katika sekta
zote ikiwemo kilimo ambacho ni uti wa mgongo kwa mataifa mengi,
Tanzania ikiwemo.

Alitoa mfano wa Tanzania kwa kusema asilimia 95 ya mizigo mizito
husafirishwa kwa njia ya barabara huku asilimia mbili pekee
ikisafirishwa kwa reli na hivyo taifa kulazimika kutumia fedha nyingi
kujenga na kukarabati barabara zinazoharibika mapema kutokana na
kuzidiwa na matumizi.

Awali akimkaribisha Dk Mwakyembe, Mwenyekiti wa AADFI, Peter Noni
alisema changamoto kubwa inayozikabili nchi za Kiafrika ni namna na
njia bora za kumudu kujenga miundombinu za uhakika bila kutegemea
misaada na ufadhili kutoka nchi wahisani na taasisi za fedha za
kimataifa.

Noni ambaye pia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Rasilimali (TIB),
allisema miongoni mwa mambo yanayotarajiwa kujalidiliwa na kkutafutiwa
ufumbuzi na namna ya kkutumia taasisi za fedha za ndani kugharamia
ujenzi wa miundombinu kupitia mikopo yenye masharti nafuu.

About Woinde Shizza

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 Comments:

إرسال تعليق

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia