KIDUMU BAND KUPAMBA MISS VYUO VIKUU MKOA WA ARUSHA
![]() | |||||
| Kidum akiwa |
Msechu
Msanii kutoka nchini Burundi ,Jean
Pierre(Kidum) kwakushirikiana na msanii wa nyimbo za kizazi kipya Peter
Msechu wanatarajia kuburudisha wananchi wa mkoa wa arusha na vitongoji
vyake katika shindano la kumsaka mrembo wa vyuo vikuu vya mkoani hapa
shindano linatarajiwa kufanyika June mbili
Akiongea na waandishi wahabari
muandaaji wa shindano hilo ambaye ni mkurunzi Fame city decor Gaudencia
Magessa alisema kuwa wasanii hao wanatarajiwa kutumbuiza katika usiku
huo wa kumsaka mrembo wa vyuo vikuu wa mkoa wa Arusha shindano ambalo
alisema kuwa litafanyika katika ukumbi wa naur ajijijini hapa.
Alibainisha kuwa jumla ya warembo
14 kutoka katika vyuo mbalimbali vilivyopo jijini hapa wanatarajiwa
kupanda ukumbini ambapo alisema kuwa warembo hao wametoka katika vyuo
mbalimbali ikiwemo chuo cha uhasibu arusha, chuo kikuu cha
makumira,pamoja na vyuo vingine vya jijini hapa.
Aidha alitaja zawadi ambazo
zitatolewa kwa washindi kuwa ni mshindi wa kwanza atajinyakulia kitita
cha shilingi laki 500000 ,wapili akiondoka na kitita cha shilingi laki
300000 huku mshindi wa tatu akiondoka na kitita cha shilingi 2000000.
Alitaja lengo haswa la mashindano
haya ni kumpata mrembo wa mkoa wa arusha ambaye ataenda kuwakilisha vyuo
vikuu vya mkoani hapa ambapo alisema kuwa pia wameamua kuandaa
mashindano haya wakiwa na nia ya kuweza kusaidia jamii mbalimbali za
mkuyani hapa ikiwa ni pamoja na kugawa misaada mbalimbali katika vituo
vya kulelea watoto yatima pamoja na wale wanaoishi katika mazingira
hatarishi.
"pia sisi tunasaidia watoto
yatima wale wasiojiweza na mbali na hapo tunasaidia kulipa ataq kwa
watoto ambao wanaitaji kusoma lakini hawana uwezo na huu ni mwanzo
tutaendelea kufanya hivi kila mara"alisema Gaudencia
alitoa wito kwa wananchi wa mkoa
wa arusha kujitokeza kwa wingi katika shindano hili kwani shindano hili
ni la kwanza na limeboreshwa sana huku akibaiinisha kuwa wameaandaa
burudani za aina mbalimbali
Alitaja baadhi ya wathamini
waliothamini shindano hilikuwa ni TBL kupitia kinywaji chao cha
Reds,Real metal graft,Modern supermarket,Perfect supermarket ,Sg
resort,mwandago investment,clouds fm,Trile a fm,Libeneke la kaskazini
blog,mount meru pure drinking water pamoja na kasse store
wakati huo huo kituo cha kulelea
watoto yatima cha Hope Ophans kimetoa shukurani kwa waandaaji wa
shindano hili kwa kuwapelekea msaada wa vyakula
akizungumza wakati akipokea
msaada huu lusi juma alisema kuwa wanashukuru kwa kupokea msaada huo
kutoka kwa warembo wao kwani unaweza kuwasidia katika kipindi hichi huku
akitoa wito kwa wananchi kuendelea kusaidia vituo hivi ambavyo
vinalelea watoto yatima pamoja na wale wanaoishi katika mazingira magumu
ili watoto hawa nao waweze kujisikia kama watoto wengine kwani watoto
wote ni sawa
Akikabidhi msaada huo muaandaaji
wa shindano hili gaudencia magessa alisema kuwa wameamua kuwasiadia
watoto hawa ili nao wajisikie kaa watoto wengine
"hii ni njia moja wapo ya kazi
zetu katika kipindi cha kufanya onyesho hili na litakuwa endelevu
alitaishia hapa kwani sisi tumejipanga kusaida jamii kwa ujumla"alisema
gaudencea
Alitaja baadhi ya misaada
walioyopeleka kuwa ni pamoja na mchele,sabuni ,unga wa ugali,mafuta ya
kupikia pamoja na maji ya kunywa.


0 Comments:
إرسال تعليق
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia