Balozi Gillian A. Milovanovic |
Takriban
muongo mmoja uliopita, jumuiya ya kimataifa ilifikia makubaliano ya
kudhibiti biashara haramu ya almasi inayochochea machafuko, vita na
ugaidi kwa kuweka utaratibu wa utambuzi wa vyanzo vya almasi ghafi
ujulikanao kama Kimberley Process (KP) certification scheme. Utaratibu
huu uliweka pia vigezo vinavyotakiwa kufuatwa katika uzalishaji na
biashara ya almasi ghafi. Hivi leo, ni lazima nchi zote 77 wanachama
waKimberley Process, wadau wengine katika biashara hii na jumuiya huru
ya kiraia zihakikishe kuwa mpango huu unafanyiwa marekebisho ili uendane
na mabadiliko yanayoendelea katika soko la dunia.
Waanzilishi Kimberley
Process walikubaliana kwa kauli moja kwamba ni lazima kudhibiti na
kukomesha kabisa almasi na mapato yatokanayo na biashara yake kugharimia
vitendo vya ukatili na mauaji yanayofanya na vikundi vya uasi.
Wakitambua kuwa biashara ya almasi inategemewa pia na mamilioni ya watu
katika kukimu Maisha yao, waanzilishi wa mpango huu walilenga pia katika
kuimarisha soko na mahitaji ya almasi halali kwa kulinda heshima na
hadhi ya madini haya.
Kimberley
Process umeweka viwango na mazingira ya haki katika uendeshaji wa
biashara ya almasi duniani. Bila kujali inazalishwa au kuuzwa wapi,
utaratibu wa utoaji hati maalumu kudhibitisha almasi zilikotoka
unamhakikishia mnunuzi kwamba hashiriki katika kufadhili au kugharimia
machafuko na ukatili unaofanywa na vikundi vya waasi.
Japokuwa
mpango wa Kimberley Process umekuwa na mfanikio mengi ya kujivunia,
tafsiri yake kuhusu dhana ya "almasi kutoka kwenye maeneo yenye
migogoro" haikidhi haja ya kukabiliana na Changamoto za sasa. Tafsiri
hii haiwezeshi kushughulikiwa kikamilifu kwa biashara ya almasi ghafi
inayohusiana na aina nyingine ya migogoro.
Mvuto
wa almasi na thamani yake unategemea sana usafi na uhalali wa kupatikana
kwake. Biashara nyingine nyingi duniani zimeathirika sana kutokana na
wanunuzi kususia bidhaa hizo kutokana na kutoridhishwa na michakato
mbalimbali katika uzalishaji wake. Kwa hali hiyo kuna wasiwasi kwamba
huenda soko zima la almasi likachafuliwa kutokana na kuwepo almasi
inayohusianishwa na vurugu na ukatili. Wateja wanataka kuhakikishiwa
kuwa almasi zao hazihusiani na vita na ukatili wa aina yoyote ile.
Huu ni
wakati wa kuchukua hatua. Wahusika wote katika biashara hii, kutoka
wazalishaji hadi wanunuzi wangependa kuona kuwa mijadala na makubalino
kuhusu Kimberley Process na tafsiri zake inawaondelea hofu hii,
inawajengea imani kuhusu biashara hii na kuzuia kuporomoka kwa mauzo ya
madini haya. Kwa Mpango Kimberley Process kushindwa kuchukua hatua
stahili, baadhi ya nchi au wahusika wengine katika biashara hii wanaweza
kuchukua hatua ambazo wao wenyewe wataona zinafaa katika kushughulikia
matarajio ya wateja.
Katika
majadilino ya awali na serikali mbalimbali, wahusika katika biashara ya
almasi na asasi huru za kiraia imeonekana kuwa ni lazima mabadiliko
katika Kimberley Process yalenge katika masuala muhimu yafuatayo:
* Ni
lazima utaratibu wa utoaji wa hati (Kimberley Process
Certificates) uendelee ili kuhakikisha kuwa biashara ya almasi
haihusiani na machafuko kwa namna yoyote ile: hati hii ni lazima
izingatie masuala ya haki za binadamu, uwazi katika masuala ya kifedha
na maendeleo mambo yanayoweza kuboreshwa zaidi kwa kubalishana uzoefu na
mbinu bora za kuyashughulikia (best practices);
* Hati
za Kimberley zitahusu migogoro ile tu ambayo imethibitishwa na vyombo
huru kuwa na uhusiano na almasi ghafi na sio tukio moja moja;
*
Masharti yote yaliyowekwa na Kimberley Process ni lazima yatekelezwe
katika kila eneo linalohusika na utafutaji wa almasi ghafi kama yalivyo
masharti ya udhibiti wa biashara haramu ya madini yoyote yale kutoka
katika maeneo yenye migogoro, mathalan masharti yaliyowekwa na mfumo wa
utoaji hati ya kuthibitisha vyanzo vya madini uliowekwa na Mkutano wa
Nchi za Ukanda wa Maziwa Makuu (International Conference of the Great
Lakes Region certification system).
Serikali
wanachama wa Kimberley Process, zikitiwa moyo na kuungwa mkono na
wahusika wote katika biashara hii pamoja na jumuiya huru ya kiraia,
zinaweza kushughulikia masuala haya na kuchukua hatua za kuleta
mabadiliko yatakayowezesha biashara ya almasi kuwa na mstakabali mwema.
Hivyo ni lazima sasa serikali hizo ziweke dhamira ya dhati ya kufikia
makubaliano kuhusu nini maana hasa ya almasi zenye mgogoro. Kushindwa
kufanya hivyo ni kujihakikishia migogoro na kutofanikiwa kwani suala au
madai ya mabadiliko hayataondoka.
Kuporomoka
kwa imani ya wateja kuhusu biashara ya almasi kunaweza kuwa na athari
mbaya kwa mataifa ambayo raia wake wengi ambao Maisha yao hutegemea
uchimbaji wa madini hayo au viwanda na biashara ya kuyaongezea thamani.
Hatimaye hasara ya kushindwa kuchukua hatua stahili kushughulikia
Changamoto hii itakuwa kubwa kuliko jitihada inayotakiwa hivi sasa
katika kufikia makubaliano ya kuboresha tafsiri ya almasi zenye migogoro
katika Utaratibu huu.