Serekali zimetakiwa kujikita katika teknolojia ya Biogas kama zinataka kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi na utunzaji wa mazingira, kukuza kipato cha wananchi wa kawaida kwa kutumia teknolojia hiyo.
Kauli hiyo imetolewa kwenye mkutano wa wanamtandao wa mashirika ya mipango ya Biogesi kutoka katika nchi kumi za kiafrika kujadili mpango kazi wa kipindi cha miaka mitatu iliyopita unaoendelea katika jiji la Arusha kwa wiki moja.
Mkutano huo unakutanisha wataalamu na wakuu wa miradi hiyo kujadili changamoto na mafanikio na juu ya wajibu wa serekali je ni kwa kiasi gani imetoa mchango kwa sekta hiyo ya teknolojia ya biogesi
Washiriki hao kutoka nchi za Kenya,Uganda,Rwanda,Comeroun,Benin, Zambia,Bukinafaso,Ghana,Burundi na wenyeji Tanzania na kuandaliwa na shirika la SNV lenye makao makuu yake jijini Arusha wakishirikiana na(TDBP) Tanzania Domestic Biogas Program.
Baadhi ya washiriki wengi wametoa lawama kwa serekali nyingi za kiafrika kutokuwa na mipango endelevu ya miradi mingi inayoletwa kwenye nchi zetu kwa kutoandaa bajeti ya miradi hiyo hivyo miradi hiyo inapofikia mwisho wa ufadhili kufa kifo cha mende.
Akizungumza kwenye mkutano huo Dr. Hailu Araya ISD (Institute for Sustainable Development) kutoka nchini Ethopia alisema kuwa teknolojia ya biogas imewekwa nyuma japo inainua uchumi na kutunza mazingira na kuokoa mabadiliko ya tabianchi kwenye nchi zetu.
Dkt.Araya alisema kuwa dunia inaingia kwenye mabadiliko tabianchi kwani sanyansi ya utunzaji wa mazingira imeifikisha hapo na kutanabaisha kuwa jamii itaendelea kukumbwa na hali hii hadi kurudi kwenye uhalisia wa utunzaji wa mazingira na kuacha kutumia teknolojia za kinyukilia na kutumia teknolojia asilia.
Nae mkurugenzi wa TDBP ambao ni wenyeji alisema kuwa mkutano kama huo unafanyika kila baada ya miaka mitatu na huwa ni kutoa taarifa za utafiti na shughuli za taasisi zinazojishulisha na teknolojia ya biogas kwenye nchi wanachama kujua ni changamoto gani na mafaniko wanayokumbana nayo.
Alisema kuwa mkutano huo utafanyika kwa wiki moja na kumalizika jumamosi ambapo washiriki watweza kwenda kutembelea miradi mbali mbali ilkuweza kujionea vile Tanzania inavyopiga hatua kwenye Teknolojia hiyo ya Biogas.