JESHI la polisi mkoani hapa linamshikilia kaka wa marehemu aliyefahamika kwa jina la Tajiri Losesia maarufu kwa jina la Pori (32) mkazi wa Mbuyuni wilaya ya Monduli kwa kosa la kumuua mdogo wake aitwaye Losiyeku Losesia (30) kwa kumpiga na fimbo kichwani.
Kamanda wa polisi mkoani hapa,Liberatus Sabas alisema kuwa tukio hilo limetokea agosti 26 mwaka huu majira ya saa 3;00 usiku katika eneo la Mbuyuni kata ya Mkuyuni wilayani Monduli baada ya ndugu hao kushindwa kuelewana wakati wanakunywa pombe za kienyeji.
Sabas alisema kuwa, siku ya tukio kaka wa marehemu alikuwa na mdogo wake huyo wakiwa wanakunywa pombe katika boma lao na baadaye kukatokea ugomvi uliosababisha kaka mtu kuchukua fimbo na kumpiga mdogo wake ya kichwani.
Alisema kuwa, chanzo cha ugomvi huo hakikuweza kujulikana mara moja kwani baada ya kupiga fimbo aliaanguka chini na kupoteza fahamu na baadae kufariki dunia wakati akipelekwa hospitali ya Monduli kwa ajili ya matibabu.
Aidha mtuhumiwa huyo atafikishwa mahakamani mara baada ya upelelezi kukamilika , huku mwili wa marehemu ukiwa umehifadhiwa katika hospitali ya Monduli .
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia