BREAKING NEWS

Friday, August 24, 2012

Kalala Junior Arejea Bendi Ya Twanga Pepeta Kwa Kishindo


  Kalala Junior akionesha umahiri wa kupiga Drums akiimba (kushoto) akiimba sambamba na Saleh Kupaza
 Kalala Junior (kushoto), akiimba sambamba na Kiongozi wa Bendi hiyo, Saleh Kupaza wakati wa mkutano na waandishi wa  habari jijini Dar es salaam jana
   Mwanamuziki aliyejiunga na Twanga Pepeta akitokea bendi ya Mapacha Watatu, Kalala Junior (wa pili kushoto) akiwaongoza wanenguaji wa bendi hiyo wakati wa mkutano wa kumtambulisha kwa waandishi wa habari jijini Dar es Salaam 

UONGOZI wa kampuni ya African Stars Entertainment Tanzania (ASET) umemtambulisha rasmi mwanamuziki mwenye vipaji vingi, Kalala Hamza Kalala maarufu kwa jina la Kalala Junior.

Kalala alitambulishwa kwenye mkutano na waandishi wa habari uliofanyika kwenye ukumbi wa Mango Garden ambapo mbali ya kusema kuwa amerejea kwa lengo la kuendeleza bendi yake hiyo aliyokuwa nayo kabla ya kujiunga na Mapacha Watatu.

Mwimbaji huyo maarufu alisema kwa fumbo kuwa “Koti limembana akiwa na bendi yake ya Mapacha na kuamua kulivua na kuacha kuendelea kulivaa tena” na kujiunga na Twanga.

“Nimefurahi kujiunga na Twanga tena na nimekuja na zawadi za nyimbo mbili, wimbo wa kwanza unaitwa Nyumbani ni Nyumbani ambao kwa sasa upo katika hatua ya mwisho na utatambulishwa rasmi wiki ijayo, ni wimbo ambao unazungumzia mambo mbali aliyokutana nayo katika muziki mpaka kuamua kurejea Twanga,” alisema Kalala.

Alisema kuwa ujio wake wa Twanga siyo wa kulazimishwa, bali umetokana na mapenzi yake mwenyewe na hasa akikumbuka fadhira za ASET ambapo ndipo alipata umaarufu mkubwa.

“Nawaomba wadau wa Twanga wakae mkao wa kula, kwani nimerejea kivingine na watarajie kupata mambo mengi mazuri, nitafanya zaidi ya yale niliyoyafanya zamani, lengo ni kuendelea kushika hatamu katika muziki wa dansi,” alisema Kalala ambaye vionjo vyake ‘vimewashika’ mashabiki wengi wa muziki wa dansi.

Afisa Habari wa ASET, Mohamed Pizaro alisema kuwa ujio wa Kalala umetokana na mpango wao waliouanzisha ujulikano Amsha Amsha Twanga Pepeta Nyumbani ni Nyumbani.

Pizaro alisema kuwa mpango huo ni maalum kwa kuhimarisha bendi yao na hasa kwa wanamuziki ambao wameonyesha nidhamu nzuri wakiwa chini ya ASET na sasa wanatumikia bendi nyingine.

Kiongozi msaidizi wa Twanga Pepeta, Saleh Kupaza alimpokea kwa mikono miwili mwimbaji huyo na kusema kazi ya kujihimarisha zaidi imeanza. “Karibu nyumbani, si unajua nyumbani ni nyumbani, tunaamini hata hao wengine wanajifanya vichwa ngumu, nao watarejea tu,” alisema Kupaza.

Share this:

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

 
Back To Top
Copyright © 2014 MOUNT KILI NEWS. Designed by OddThemes | Distributed By Gooyaabi Templates