BREAKING NEWS

Saturday, August 25, 2012

MARY NAALI AHAIDI KUVUNJA REKODI SAFARI MARATHON

Mwanariadha mary naali akiwa anafanyishwa mazoez i na mwalimu wake kocha denis Malle katika uwanja wa kumbukumbu ya Sheikh Amri Abeid
mwanariadha maarufu toka mkoani Arusha ambaye ndie aliweza kutetea  nchi yake katika mashindano ya safari marathon Mary Naaly amesema kuwa atahakikisha katika kipindi hichi cha mashindano  hayo ambayo ufanyika mkoani hapa anavunja rekodi ya mwaka jana

Mwanariadha huyo ambaye katika mashindano yaliyopita aliweza kushika nafasi ya kwanza katika mbio za wanawake za kilometa 21 ambapo aliweza kukimbia kwa kutumia muda wa 1:14:02 na kuweza kuwapita wanaridha wengine kutoka nchini kenya  aliyasema hayo wakati akifanya mazoezi ya kujiandaa na mashindano hayo  katika uwanja wa kumbukumbu za sheikh Amri Abeid jijini hapa.


mary naali alisema kuwa  katika mashindano hayo ya safari marathoni ambayo yanatarajiwa kufanyika september tisa mwaka huu jijini hapa anaimaini kabisa ataweza kukimbia vyema na kuwashinda wanariadha wengine ambao watashiriki.


Kwa upande wake mwalimu wa mwanariadha huyu Denes Malle alisema kuwa yeye kama kocha wa mwanariadha huyu anauwakika kabisha mchezaji wake ataweza kukimbia nakuvunja rekodi ya mwaka jana ambayo yeye mwenyewe ndio aliyoiweka .


Alisema kuwa amekuwa akimpa mwanariadha huyu mazoezi ya aina mbalimbali  ya kujiandaa ili aweze kushinda katika mashindano haya.


Mashindano haya ya safari marathoni yamekuwa yakifanyika jijini Arusha kilamwaka na yanashirikisha wanaridha kutoka sehemu mbalimbali ikiwemo kenya ,uganda,rwanda  ,Burundi pamoja na Ethiopia.


Katika mashindano yaliyopita Mtanzania pekee aliyoweza kufanya vyema alikuwa mary Naali ambapo ndie alikuwa mshindi wa kwanza wa mbio za wanawake kwa kilometa 21 akifuatiwa na wakenya ambao walishikilia nafasi ya pili adi ya tano huku kwa upande wa wanaume wakenya hao hao ndio walishikilia nafasi zote.

Share this:

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

 
Back To Top
Copyright © 2014 MOUNT KILI NEWS. Designed by OddThemes | Distributed By Gooyaabi Templates