VIONGOZI WA VIJIJI NA KATA WATAKIWA KUSIMAMIA MIRADI YA MAENDELEO

Mkuu wa wilaya ya Hai Bwana Novatus Makunga  amewaagiza viongozi wa vijiji na kata kusimamia miradi ya maendeleo sanjari na kudai stakabadhi zinazoonyesha kiasi cha fedha zinazotumika katika miradi inayoanza kutekelezwa katika maeneo yao.

Makunga ametoa agizo hilo baada ya kukagua  ujenzi wa barabara  ya kilometa sita na nusu  ya vijiji vya kata ya machame Mashariki,inayounganisha njia panda ya Makoa na vijiji vya  Nkuu Sinde,Foo na Nronga inayojengwa na serikali kwa Sh.Milioni 20 kwa
kiwango cha Moramu.

Amewataka viongozi wa vijiji kusimamia kila mradi unaotambulishwa katika vijiji vyao kwa kuwa na nyaraka zinazoonyesha aina ya mradi na idadi ya vifaa vitakavyotumika ili kudhibiti vitendo vya uchakachuaji wa miradi hiyo.

Akizungumza kwa niaba ya wananchi wa vijiji hivyo bw.Isaya Mlengeni ameeleza uwa, kabla ya ujenzi wa barabara hiyo,walikuwa wanatembea umbali mrefu kwa miguu kutokana na ubovu wa barabara hiyo.

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

Previous Post Next Post