WASHAURIWA KUSOMA MAPATO NA MATUMIZI

VIONGOZI wa kata na vijiji wilayani Meru, wameagizwa kuitisha mikutano mikuu kwa mjibu wa katiba ili kusoma mapato na matumizi sanjali na kuwaeleza wananchi  utekelezaji wa miradi mbalimbali na kuondoa manung’uniko ambayo yanasababisha lawama zisizokuwa za lazima kwa Chama na serikali yao..

Agizo hilo limetolewa jana na Katibu wa CCM, wilaya ya Meru, mkoani Arusha, Langael Akyoo, alipokuwa akihutumbia mkutano wa hadhara uliofanyika eneo la Sokoni katika kijiji cha Kikatiti mara baada ya kuzindua tawi jipya la Nashoni.

Katibu huyo amesema viongozi wa ngazi za Kata na vijiji wamekuwa hawaitishi mikutano na kuwasomea wananchi mapato na matumizi na matokeo yake ni kuwepo kwa hasira za wananchi dhidi ya Serikalki na Chama cha Mapinduzi kwa kudhania kuwa ndivyo  vyanzo vya kutokusomewa  taarifa za mapato na matumizi .

Akyoo, ametolea mfano kwenye baadhi ya shule za msingi na sekondari, ambako bodi na kamati za shule huwa haziitishi mikutano  na badala yake zinatoa maamuzi ya michango mikubwa bila kuwashirikisha wazazi hali ambayo inasababisha chuki na hasira dhidi ya serikali na Chama.

Akyoo,amesema maamuzi hayo pia yamekuwa yakihusisha wanafunzi wanaojiunga na sekondari kila mwaka kuchangia madawati, meza na viti na hiyo ni baadhi ya kero ambazo zinawaumiza wananchi na hasira zao wanazimalizia kwa kukisulubu  Chama cha mapinduzi wakati wa uchaguzi mkuu .

Amesema kuwa serikali za viji zimekuwa zikipokea fedha toka halmashauri na zinafanya maamuzi bila kuwashirikisha wananchimatokeo yake  kuibuka kwa malamiko ambayo huwa hawapatiwi ufumbuzi wake.

Akasema kuwa anashangaa kuona hayo yote yanafanyika huku viongozi mbalimbali wakiwemo Madiwani na wenyeviti wa vijiji na vitongoji wakiwepo bila kuchukua hatua na hiyo inaonyesha wameshindwa kuwajibika hivyo akawatahadharisha kubadilika vinginevyo Chama cha Mapinduzi hakitawavumilia.


“Ninawaagiza madiwani na wenyeviti wa vijiji na vitongoji kuhakikisha mnafuatilia  kero hizo ,tusitafute wachawi wanaosababisha CCM, kuchukiwa wakati wachawi ni nyie wenyewe”alisema Akyoo.

Akaagiza wataalamu wa ugani wa Kilimo, na mifugo katika vijiji kuhakikisha wanakwenda kwenye maeneo ili kutoa elimu kwa wananchi na badala ya kukaa maofini huku wananchi wakikosa huduma na madiwani wasimamie kutatua kero hizo na atakae shindwa kutimiza wajibu wake aondoke katika utumishi kabla hajatimuliwa.

Wananchi wanakiamini Chama chao kuwa kipo kwa ajili ya kuwatetea lakini kero  zisipotatuliwa wanajenga chuki tunataka tufike sehemu wananchi waridhike na huduma zinazotolewa .

Kuhusu ombi la kuanzishwa kijiji kingine kwa ajili yakurahisisha huduma kutokana ukubwa wa kijiji hicho cha Kikatiti, Katibu huyo amewaagiza viongozi na wananchi hao waanze mchakato huo ili kijiji kipya kiweze kupatikana mapema .

Kuhusu tatizo la maji katika kata hiyo, Katibu huyo amewahakikishia wananchi hao kwamba hiyo ni miongoni mwa kero kubwa zilizopo na akaahidi kufuatilia  ili maji yaweze kupatikana kijijini hapo na kutosheleza mahitaji

Awali akito ufafanuzi wa kutokuwepo kwa umeme katika eneo hilo, makamu mwenyekiti wa halmashauri ya Meru, Diwani Frida Kaaya, amewaambia wananchi hao kuwa halmashauri ya wilaya imetenga kiasi cha shilingi milioni 52 kwa ajili ya kusambaza umeme eneo hilo na kinachosubiriwa ni utekelezaji kutoka Tanesco.

Kuhusu vikundi vya uzalishaji mali, makamu mwenyekiti huyo amesema vipo na akatoa wito kwa akina mama kuanzishavikundi vingine zaidi vya kiuchumi ili waweze kupataiwa mikopo ya fedha kutoka halmashauri ,mfuko wa jimbo na benki ya wananchi wa Meru.

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

Previous Post Next Post