JAMBAZI AWAWA ARUSHA


mtu asiyefahamika jina, mwanaume anayekadiriwa kuwa na umri kati ya miaka 28 na 30 ambaye anadhaniwa kuwa ni jambazi alifariki dunia akiwa njiani anapelekwa hospitali kwa ajili ya matibabu baada ya kupigwa risasi na askari polisi mara baada ya kukahidi amri halali ya kujisalimisha.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na kamanda wa polisi mkoani Arusha lebaratu sabas alisema kuwa tukio hilo lilitokea  mnamo tarehe 13/08/2012 muda wa saa 8:30 usiku katika kijiji cha levorosi kata ya kimnyaki wilayani arumeru.
Alibainisha kuwa tukio hilo lilitokea wakati askari wa jeshi la polisi na jambazi huyo ambaye kwa sasa ni marehemu wakijibizana kwa kurushiana risasi na hivyo askari kufanikiwa kumpiga risasi tumboni na mara baada ya upekuzi walifanikiwa kumkuta akiwa na bunduki aina ya rifle 458 yenye namba7052602464 model zkk-620 ambaye ilikuwa imekatwa mtutu pamoja na kitako ikiwa na risasi mbili.
Aidha alisema kuwa awali askari hao walikwenda katika nyumba ya marehemu na kuizingira na marehemu alishtuka baada ya kusikia milio ya mbwa na akafungua mlango  na mara alipogundua kuna askari alianza kuwarushia risasi mbili ili apate njia ya kutoroka japokuwa  alipewa amri halali ya kujisalimisha lakini alikaidi.
Sabas alisema kuwa uchunguzi wa jeshi la polisi ulibaini kwamba  marehemu alikuwa  anashirikiana na wenzake katika matukio mbalimbali ya uhalifu na jitihada za jeshi la polisi zilifanikiwa kuwakamata watuhumiwa watatu ambao walikuwa wanashirikiana na marehemu katika matukio ya uhalifu yaliyofanyika katika maeneo tofauti ya nchi.
“tulivyowahoji watuhumiwa hao  walikiri kushirikiana na marehemu katika matukio mbalimbali na kueleza anapoishi, ndipo askari walipoendelea na upelelezi na siku hiyo ya agosti  13 walifanikiwa kuizingira nyumba hiyo ambapo kulitokea majibizano ya risasi na hatimaye mtuhumiwa kupigwa risasi ya tumbo na kufariki dunia akiwa anapelekwa hospitali kwa ajili ya matibabu.
Alisema kuwa mara baada ya kuipata bunduki hiyo kutoka kwa marehemu katika uchunguzi askari  waligundua kwamba, bunduki iliyokuwa inatumiwa na marehemu pamoja na wenzake iliporwa toka kwa mtu aliyefahamika kwa jina la gabriel  william mkazi wa sekei april  moja majira ya  saa 4:00 usiku ambapo mmiliki huyo alivamiwa na majambazi hao akiwa anaingia katika geti la nyumba yake huku akiwa na gari yake aina ya suzuki escudo yenye namba za usajili t. 887 apc.
Katika tukio lingine bunduki moja aina ya short gun-greeners gp gun  imekutwa ikiwa imefutwa namba baada ya watu wanaoaminika kuwa ni majambazi kuitelekeza baada ya kugundua kuwa wanafuatiliwa na askari.
 Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo kamanda wa polisi mkoani hapa Lebarutus sabas alisema kuwa tukio hilo lilitokea huko ilboru agosti  mbili usiku ambapo askari wa jeshi la polisi mkoani hapa wakiwa doria walifanikiwa kukamata bunduki hiyo.

Alisema kuwa askari hao waliokuwa doria   kulitilia shaka kundi la watu hao na mara baada ya kundi hilo kugundua kwamba ni askari polisi walianza kukimbia na mmoja wao kutupa chini  mfuko mweusi na mara baada ya askari kuupekuwa waliona begi dogo ambapo ndani yake waliikuta bunduki hiyo ambayo ilikuwa imekatwa mtutu na kitako ikiwa na risasi 12.
mpaka hivi sasa watuhumiwa hao bado hawajapatikana na jeshi la polisi linaendelea na juhudi za kuwatafuta. mafanikio hayo yametokana na msako endelevu ulioanza toka agosti sita  mwaka huu katika maeneo mbalimbali ya mkoa huu.  

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

Previous Post Next Post